Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mwanaisha Ng'anzi Ulenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara inayoanzia Makutano ya Kiomomi hadi Makutano ya Mlingano – Tanga kwa Kiwango cha lami?

Supplementary Question 1

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, ninaishukuru Serikali walau kwa kuanza usanifu na upembuzi yakinifu wa Barabara ya Bypass ya Tanga. Ninayo maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, lengo la ujenzi wa Barabara za Bypass ni kuzipunguzia msongamano barabara kuu, sambamba na kuhakikisha barabara zinakuwa katika hali nzuri, je, nini mkakati wa Serikali kumaliza Barabara ya Tanga – Pangani ili kufikia malengo tarajiwa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Barabara niliyoitaja ya Tanga – Kiomoni – Mlingano iko parallel na Barabara ya Tanga – Segera. Je, ni nini mkakati wa Serikali wa kuipanua Barabara ya Tanga – Segera, ambayo sasa imezidiwa? Ahsante sana.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, mkakati wa Serikali kukamilisha Barabara ya Tanga – Pangani upo pale pale na unaendelea. Hii barabara inajengwa kwa kiwango cha lami, kilometa 50, ambapo sasa hivi tuko zaidi ya 50%. Ninamhakikishia Mheshimiwa Ng’anzi Ulenge kwamba, hiyo barabara tutaikamilisha ikiwa ni mpango wa kuunganisha Tanga hadi Makurunge (Bagamoyo). Ujenzi unaendelea kwenye lots nyingine.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Barabara ya Tanga – Segera, tunavyoongea sasa hivi, nadhani hata kwenye bajeti tumeelezea kwamba, tuko kwenye hatua ya kumtafuta mhandisi mshauri ili aweze kuisanifu hiyo barabara tuweze kuipanua, na hasa kufuatia mafanikio makubwa sana ambayo Bandari ya Tanga inayo. Pia, ndiyo inayosababisha kutengeneza hiyo bypass, lakini bypass hiyo lazima iendane na upanuzi wa Barabara ya kutoka Tanga kwenda Segera, ahsante.