Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 34 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 406 | 2026-05-21 |
Name
Mwanaisha Ng'anzi Ulenge
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga Barabara inayoanzia Makutano ya Kiomomi hadi Makutano ya Mlingano – Tanga kwa Kiwango cha lami?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Mhandisi Mwanaisha Ng’anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi, kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), inaendelea na kazi ya usanifu wa Barabara ya Makutano ya Mlingano – Mjesani – Pande – Kiomomi pamoja na barabara ya Geza – Pongwe – Pande (Tanga Bypass), kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami. Baada ya kazi ya usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved