Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Rebeca Sanga Nsemwa
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. REBECA S. NSEMWA K.n.y. MHE. FESTO R. SANGA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Nkenja – Usalimwani inayounganisha Kata ya Mfumbi na Kitulo kwa kiwango cha changarawe?
Supplementary Question 1
MHE. REBECA S. NSEMWA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali. Kwa kuwa, hali ya barabara hiyo kwa sasa ni mbaya sana kutokana na mvua nyingi zilizonyesha, je, ni nini kauli ya Serikali ya kufanya matengenezo ya dharura kwa barabara hiyo, ili wananchi wa Wilaya ya Makete waendelee na shughuli zao za kiuchumi, ukizingatia hao ni wakulima hodari na wafanyabiashara maarufu nchini Tanzania?
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Mkandarasi anayejenga Barabara ya Matamba Mjini kilometa moja na meta 800, ameondoka site muda mrefu, licha ya kuwa amelipwa fedha zake. Je, ni nini kauli ya Serikali kwa mkandarasi huyo? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli eneo ilipo barabara hii ni la miinuko na lina mvua nyingi. Barabara hii ndiyo kwanza imepanda hadhi kuja TANROADS. Kwa hiyo, tunachofanya, kwanza, ni kuhakikisha kwamba tunaitoa katika hali iliyokuwa na kuileta kwenye viwango vya TANROADS. Ndiyo maana tumeamua kwanza kukarabati na kutengeneza yale maeneo korofi ili iweze kupitika, lakini mpango ukiwa ni kuitengeneza barabara yote.
Mheshimiwa Spika, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge na ninatoa maelekezo hapa kwa Meneja wa TANROADS kwamba, mvua imepungua sana katika maeneo hayo, aweze sasa kuitembelea hiyo barabara ili yale maeneo yote ambayo yanafanya wananchi wasiweze kupita kwenye hiyo barabara, basi aweze kuyatengeneza kwa sababu, mkandarasi ambaye amepangiwa hiyo kazi, yupo.
Mheshimiwa Spika, kuhusu Barabara ya Matamba – Mjini; kwa kuwa, mkandarasi amelipwa na nina hakika mvua imepungua, Meneja wa Mkoa wa Njombe ahakikishe kwamba, mkandarasi anarudi na kukamilisha hiyo kazi ambayo amepewa na Serikali, ahsante.
Name
Josephine Joseph Kapoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. REBECA S. NSEMWA K.n.y. MHE. FESTO R. SANGA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Nkenja – Usalimwani inayounganisha Kata ya Mfumbi na Kitulo kwa kiwango cha changarawe?
Supplementary Question 2
MHE. JOSEPHINE J. KAPOMA: Mheshimiwa Spika, Wananchi wa Wilaya ya Gairo, Mkoani Morogoro, wanashukuru sana kwa kupatiwa Madaraja ya Chakwale na Nguyami yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 24, lakini sasa tuna Daraja dogo sana la Matare ambalo linaunganisha Idibo na kuelekea Kilindi, Tanga na kata nyingi za Gairo, ambalo tumeliomba kwa muda mrefu sana. Ni lini Serikali itatukumbuka kukamilisha ujenzi wa daraja hili? Ahsante.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mpango wa kutengeneza yale madaraja ambayo yalikuwa changamoto miaka yote, na yale aliyoyataja Mheshimiwa Mbunge, ya Chakwale na Nguyami, yamekamilika na sasa wananchi hao wanapita.
Mheshimiwa Spika, hiyo barabara tunavyoongea sasa hivi ipo kwenye mpango wa kusanifiwa, ikiwa ni pamoja na hilo daraja. Ninamwelekeza tu Meneja wa Mkoa wa Morogoro aweze kwenda kwenye hilo eneo, ili wakati tunakamilisha usanifu, basi tuweze kupata mahitaji na kuona uwezekano wa kulitengeneza hilo daraja kwa muda; kwa sababu, madaraja yale makubwa yametengenezwa, basi na hilo tuweze kuliangalia kama linaweza likatengenezwa kwa udharura, kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge, ahsante.
Name
Kija Limbu Ntemi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Katoro
Primary Question
MHE. REBECA S. NSEMWA K.n.y. MHE. FESTO R. SANGA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Nkenja – Usalimwani inayounganisha Kata ya Mfumbi na Kitulo kwa kiwango cha changarawe?
Supplementary Question 3
MHE. KIJA L. NTEMI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kumwuliza Mheshimiwa Waziri swali. Barabara ya kutoka Chibingo kwenda Chigunga kwenda Bukondo iko chini ya TANROAD, lakini kwa kiwango cha changarawe. Barabara hiyo ni mbovu sana kwa sasa na wananchi wetu wanapata shida kupita katika ile barabara. Je, kwa kuwa mvua imeisha, nini kauli ya Serikali kwa sasa ili watu wetu waweze kupita vizuri katika ile barabara? Ahsante.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba, barabara ambazo ni za changarawe katika kipindi cha mvua huwa zinakuwa na changamoto maeneo mengi, na baada ya mvua kukatika wakandarasi wanarudi site. Ninamwelekeza Meneja ahakikishe kwamba hiyo barabara mkandarasi arudi site aweze kuitengeneza, na hasa akianza na yale maeneo ambayo yameharibika zaidi ili wakati anatengeneza barabara yote wananchi waendelee na maisha yao ya kawaida, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved