Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 34 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 405 | 2026-05-21 |
Name
Festo Richard Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. REBECA S. NSEMWA K.n.y. MHE. FESTO R. SANGA aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Nkenja – Usalimwani inayounganisha Kata ya Mfumbi na Kitulo kwa kiwango cha changarawe?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Festo Richard Sanga, Mbunge wa Makete, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ukarabati wa Barabara ya Nkenja – Usalimwani (kilometa 42.7) kwa kiwango cha changarawe unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Hadi sasa matengenezo makubwa yamefanyika katika sehemu korofi za maeneo ya vitongoji vya Nkenja na Ikuwo. Aidha, Serikali imepanga kuendelea na kazi za kuweka changarawe katika maeneo ya mlima yaliyopo Kitongoji cha Usalimwani na maeneo mengine yaliyobaki, ili kuhakikisha barabara hiyo inapitika majira yote ya mwaka, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved