Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Abubakar Mohammed Mussa Sururu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtoni
Primary Question
MHE. ABUBAKAR M. MUSSA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ku-print Vitambulisho vya NIDA Zanzibar kama ilivyo Passport ili kurahisisha upatikanaji wa vitambulisho hivyo kwa Wananchi?
Supplementary Question 1
MHE. ABUBAKAR M. MUSSA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kuniruhusu niulize swali la nyongeza. Nina swali moja tu. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, je, haioni haja sasa kuanzisha kituo kidogo cha ku-print vitambulisho hivyo Zanzibar, ambacho kitakuwa na hadhi sawa za kiusalama, kama hicho kilichopo huku Tanzania Bara? Ahsante.
Name
Mohammed Mahmoud Ayoub
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chaani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ninamshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Abubakar kwa hoja yake hiyo ya msingi na muhimu. Serikali inaona haja ya kufanya hivyo, lakini inazingatia zaidi dhana ya usalama, udhibiti wa ubora na kuepusha udanganyifu.
Mheshimiwa Spika, hii ni kutokana na umuhimu wa Kitambulisho cha Taifa kwani, Kitambulisho cha Taifa kina utofauti mkubwa na hati ya kusafiria (passport). Kitambulisho cha Taifa ndicho kinacholinda Utanzania na uasili wetu. Kwa hiyo, ni kitu ambacho kiukweli siyo cha kuchezea hata kidogo. Kwa mnasaba huo, pale ambapo haja na hoja itaonekana ya kufanya hivyo, Serikali itafanya hivyo. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved