Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 34 | Home Affairs | Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi | 404 | 2026-05-21 |
Name
Abubakar Mohammed Mussa Sururu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtoni
Primary Question
MHE. ABUBAKAR M. MUSSA aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ku-print Vitambulisho vya NIDA Zanzibar kama ilivyo Passport ili kurahisisha upatikanaji wa vitambulisho hivyo kwa Wananchi?
Name
Mohammed Mahmoud Ayoub
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chaani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Abubakar Mohammed Mussa, Mbunge wa Jimbo la Mtoni, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, uzalishaji wa Vitambulisho vya Taifa nchini hufanyika katika Kituo Kikuu cha Uchakataji wa Taarifa (Data Centre-DC) ambapo taarifa zote za usajili na utambuzi wa watu wote waliosajiliwa huchakatwa kwa ajili ya kuzalisha Namba ya Utambulisho (NIN) na Vitambulisho. Kituo hicho kina miundombinu mbalimbali ya kuwezesha utambuzi wa mwombaji na ulinganifu wa alama za vidole (Automated Fingerprint Identification System) ambao unamtambua kipekee mwombaji wa Kitambulisho cha Taifa.
Mheshimiwa Spika, uchapishaji wa Vitambulisho vya Taifa hufanyika kwa mfumo wa jumla (Centralized System) ili kuhakikisha usalama, udhibiti madhubuti wa ubora, pamoja na usimamizi thabiti wa taarifa muhimu za wananchi wanaosajiliwa na kutambuliwa. Uchapishaji wa vitambulisho katika kituo kimoja chenye ulinzi na udhibiti husaidia katika ulinzi wa taarifa za kibayometriki, mifumo ya usimbaji (encryption) na vifaa maalum, na hivyo kupunguza hatari ya udanganyifu, uvujaji wa taarifa na au utengenezaji wa vitambulisho bandia (fraud), uwezekano wa kutofautiana kwa ubora wa vitambulisho, pamoja na ongezeko la gharama za uendeshaji kutokana na hitaji la mitambo na rasilimali watu katika maeneo yatakayoanzishwa vituo. Ninaomba kuwasilisha, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved