Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Charles Jacob Sungura
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Vijijini
Primary Question
MHE. DKT. CHARLES J. SUNGURA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga viwanda vya kuchakata nyama na maziwa katika Jimbo la Handeni kwa kuwa lina wafugaji wengi wa ng’ombe, mbuzi na kondoo?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. CHARLES J. SUNGURA: Mheshimiwa Spika, ninaomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa Kiwanda cha Maziwa cha Tanga Fresh ambacho kilikuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Handeni pamoja na mkoa wa ujumla, lakini sasa hivi uzalishaji umesimama. Je, Serikali ina mpango gani sasa kuhakikisha kwamba kiwanda hicho kinarejea katika uzalishaji ili kiwe mkombozi kwa ajili ya wananchi wa Handeni na Mkoa wa Tanga kwa ujumla? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa maeneo ya Segera Kabuku na Kwamgwe katika Jimbo la Handeni yanasifika sana kwa kilimo cha machungwa. Ninaomba kauli ya Serikali, ni lini sasa itajenga kiwanda cha kuchakata machungwa katika maeneo haya kwa sababu 50% ya machungwa yanayolimwa katika maeneo haya yanakuwa yakioza shambani kwa kukosa soko, na pia kwa kukosa viwanda vya kusindika machungwa hayo? Ninashukuru sana. (Makofi)
Name
Denis Lazaro Londo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mikumi
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, kwanza, nikiri kwamba Mkoa wa Tanga ni moja ya mikoa ambayo imebarikiwa sana kwa mazao ya mifugo. Kuhusiana na Kiwanda cha Tanga Fresh, ninaomba nikiri kwamba ni kweli kuna changamoto za kiuendeshaji wa kiwanda hicho. Kiwanda hiki kina uwezo wa kuzalisha maziwa lita 120,000 kwa siku na ndiyo soko kuu na la uhakika kwa ajili ya bidhaa za maziwa kutoka Tanga na mikoa ya jirani.
Mheshimiwa Spika, hivi sasa Serikali, kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Chama cha Ushirika wa Wazalishaji Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU), Hazina na Wizara ya Kilimo, wako kwenye mchakato wa kuona namna bora ya kufufua shughuli za kiwanda hiki na kuimarisha uzalishaji wa maziwa.
Mheshimiwa Spika, Serikali, kupitia Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Tume ya Maendeleo ya Ushirika, ameunda timu ambayo inaandaa ripoti na Jumatatu itaiwasilisha ripoti hiyo ili kuona namna bora ya kuimarisha shughuli za uzalishaji na kuzindua ama kuhamasisha shughuli za uzalishaji. Hata hivyo, tunahamasisha sekta binafsi kuendelea kujitokeza kuongeza idadi ya viwanda kwa ajili ya kuongeza thamani ya maziwa.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala la matunda, ni kweli, tathmini imefanywa miongoni mwa mazao ya uhakika mkoani Tanga ama maeneo ya kimkakati ambayo tunaweza tukaweka viwanda pamoja na kuongeza thamani ya bidhaa za nyama na maziwa katika mkoa huo, na pia, bidhaa za matunda katika Wilaya ya Korogwe na Muheza. Hivyo, hamasa inaendelea kwa sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika uwekezaji wa kimkakati katika mkoa huu, hasa katika maeneo ya kuongezea thamani mazao ya matunda. Ninaomba kuwasilisha.
Name
Ado Shaibu Ado
Sex
Male
Party
ACT
Constituent
Tunduru Kaskazini
Primary Question
MHE. DKT. CHARLES J. SUNGURA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga viwanda vya kuchakata nyama na maziwa katika Jimbo la Handeni kwa kuwa lina wafugaji wengi wa ng’ombe, mbuzi na kondoo?
Supplementary Question 2
MHE. ADO S. ADO: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi, ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa Serikali ilitoa ahadi katika Bunge hili, kupitia swali la msingi nililoliuliza kwamba inao mpango wa kuhakikisha Kiwanda cha Kubangua Korosho Tunduru maarufu kama Kiwanda cha Bias, kitaanza kufanya kazi katika msimu wa mavuno ya korosho wa mwaka huu; na kwa kuwa imebaki miezi michache kwa msimu wa mavuno ya korosho kuanza, ni ipi kauli ya Serikali juu ya hatua iliyofikiwa ili kuhakikisha kwamba ahadi hii inatekelezwa kwa vitendo? Ahsante.
Name
Daniel Godfrey Chongolo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makambako
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni kweli kulikuwa na ahadi ya huyu mwekezaji kuanza uzalishaji wa kubangua korosho katika msimu huu. Tumemwita Wizarani ili atuambie amefikia wapi? Kwa sababu kuna commitment ambayo tumeweka na wananchi wanasubiria kule kuona kwamba uzalishaji wa korosho unaendelea, na pia commitment yake inaheshimiwa. Ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved