Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 34 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 403 2026-05-21

Name

Charles Jacob Sungura

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Vijijini

Primary Question

MHE. DKT. CHARLES J. SUNGURA aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga viwanda vya kuchakata nyama na maziwa katika Jimbo la Handeni kwa kuwa lina wafugaji wengi wa ng’ombe, mbuzi na kondoo?

Name

Denis Lazaro Londo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mikumi

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara, ninaomba sasa kujibu swali Na. 403 kama lilivyoulizwa na Mheshimiwa Charles Jacob Sungura Mbunge wa Handeni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika Jimbo la Handeni Mjini, kuna Kiwanda kimoja kidogo cha kuchakata na kusindika maziwa kiitwacho Bin Maweni Fully Milk Processing. Kwa sasa Serikali imeshatenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vingine vya kuchakata mazao ya mifugo. Maeneo hayo ni Kwamagome, Ngugwini na Mabanda. Serikali inaendelea na juhudi za kutafuta wawekezaji mahiri kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo ikiwemo nyama na maziwa. Ninaomba kuwasilisha.