Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mariam Nassoro Kisangi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Temeke
Primary Question
MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kituo cha Afya katika Kata ya Sandali Jimbo la Temeke?
Supplementary Question 1
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, kwanza, ninaipongeza sana Serikali kwa hatua hiyo na majibu hayo yenye kuridhisha na kuleta matumaini kwa wananchi wa Kata ya Sandali. Ombi langu, ninaomba hayo ambayo yamepangwa au huo mchakato, utekelezwe kwa haraka.
Mheshimiwa Spika, swali nililonalo sasa, je, kwa kuwa changamoto Kata ya Sandali inayopitia katika Jimbo la Temeke inapitia Kata ya Azimio, na Kata ya Azimio ina wananchi 63,836 kwa mujibu wa sensa, lakini wana zahanati ndogo sana na hawana kituo cha afya, Serikali haioni umuhimu sasa wa kujenga vituo vya afya hasa kwenye maeneo ambayo yana wananchi wengi? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Mariam Nassoro Kisangi, Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa ufuatiliaji wa dhati kabisa wa ustawi na maendeleo ya Wananchi wa Jimbo la Temeke, na tukuhakikishie tu kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, tutaendelea kukupa ushirikiano kuhakikisha wananchi wa Jimbo la Temeke wananufaika na matunda ya Serikali hii. (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, mpongeze na Mkurugenzi wa Ilala. (Makofi/Kicheko)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, kwa hakika, na siku mbili zilizopita nilimpongeza sana Mkuu wa Wilaya, Mpogolo, na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma, wanafanya kazi nzuri sana ya kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Ahsante sana. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba, tayari tumeshatenga fedha hii shilingi bilioni 2.5 kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. Nitumie nafasi hii kurejea kumpongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, amekuwa Mkurugenzi wa mfano wa kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya kuboresha huduma katika jamii na wananchi anaowaongoza.
Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikitoa maelekezo mara kwa mara kwamba Wakurugenzi pamoja na fedha za Serikali Kuu watumie pia fedha za mapato ya ndani katika ujenzi wa miundombinu kama zahanati, madarasa na vituo vya afya. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pili, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Kata hii ya Azimio na maeneo mengine ambayo tutafanya tathmini na kuona vigezo, moja ikiwa idadi ya watu ambayo mmeshaisema inatosheleza; na pili, umbali kutoka kituo cha karibu zaidi ili tuweze aidha kupandisha hadhi ya Zanahati ya Azimio kuwa kituo cha afya kulingana na eneo ambalo litapatikana.
Name
Dickson Nathan Lutevele
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafinga Mjini
Primary Question
MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kituo cha Afya katika Kata ya Sandali Jimbo la Temeke?
Supplementary Question 2
MHE. DICKSON N. LUTEVELE: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kata ya Isalavanu ni Kata ambayo iko pembezoni sana katika Kata za Halmashauri ya Jimbo la Mafinga Mjini, lakini ndiyo kata pekee kwenye jimbo hili ambayo haina kituo cha afya mpaka leo. Ninaomba kujua Serikali ina mpango gani wa ujenzi wa kituo cha afya kwenye Kata hii ya Isalavanu hasa ukizingatia kwamba wamekidhi vigezo vyote? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ni kweli Kata ya Isalavanu katika Jimbo la Mafinga Mjini iko pembezoni. Nitumie nafasi hii nimhakikishe Mheshimiwa Mbunge kwamba tutawasiliana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga ili wawasilishe rasmi taarifa ya vigezo vya kata hiyo kwa mujibu wa mwongozo wetu; na ikiwa itakidhi vigezo, tutakubaliana kwanza kuanza kutenga mapato ya ndani ya halmashauri kwa awamu, wakati Serikali kuu inatafuta fedha kwa ajili ya kwenda kuunga mkono na kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved