Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 34 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 401 2026-05-21

Name

Mariam Nassoro Kisangi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Temeke

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kituo cha Afya katika Kata ya Sandali Jimbo la Temeke?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mariam Nassoro Kisangi, Mbunge wa Jimbo la Temeke, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2026/2027 Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, imetenga shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Sandali kwa muundo wa ghorofa. Aidha, wataalamu ngazi ya Mkoa na Manispaa wanakamilisha uandaaji wa michoro na kuwasilisha Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeweka kipaumbele cha kukamilisha miradi viporo ya Vituo vya Afya 364 kote nchini ili viweze kutoa huduma stahiki zikiwemo huduma za dharura za upasuaji, ahsante.