Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Sheila Edward Lukuba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SHEILA E. LUKUBA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Shule mpya za Sekondari katika Kata za Mawasiliano na Luhungo ili kupunguza msongamano wa wanafunzi?

Supplementary Question 1

MHE. SHEILA E. LUKUBA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, ninaomba niulize maswali madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, tumebakiza mwezi mmoja kukamilisha mwaka wa Serikali wa 2025/2026. Je, lini Serikali itatoa fedha ili kuweza kwenda kujenga shule iliyopo Mtaa wa Mawasiliano?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga mabweni kwenye shule ambazo zimeshajengwa na ambazo zinaendelea kujengwa ili kusaidia wanafunzi hasa wanaotoka maeneo ya mbali? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Sheila Edward Lukuba, Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Morogoro kwa namna anavyowasemea na kuwawakilisha vyema sana wananchi wa Mkoa wa Morogoro na Watanzania kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, tayari wiki hii Jumatatu tumeshapeleka exchequer ya kupeleka hii shilingi 528,000,000 katika Kata ya Mkundi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Shule ya Sekondari Mawasiliano. Kwa hiyo, nimhahikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba fedha hiyo itakwenda kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Tano ili kazi za ujenzi ziweze kuanza.

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Mpango wa Serikali ni kujenga mabweni kwanza kwenye shule za kidato cha tano na sita kwa sababu zinachukua wanafunzi wa Kitaifa, na pili kwenye shule za O-level ambazo zina changamoto za kimazingira. Kwa mfano, kwa maeneo ya wafugaji ambao watoto wanalazimika kutembea umbali mrefu sana kwenda shule, basi maeneo haya na maeneo mengine yenye sababu za kijiografia, tumekuwa tukitenga fedha kwa ajili ya kujenga mabweni.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kujenga mabweni katika shule zetu na kuhakikisha kwamba watoto wetu wanasoma katika mazingira bora zaidi.

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. SHEILA E. LUKUBA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Shule mpya za Sekondari katika Kata za Mawasiliano na Luhungo ili kupunguza msongamano wa wanafunzi?

Supplementary Question 2

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, toka mwaka 2024 tulikuwa na ujenzi wa Shule ya Sekondari Kurusanga na Mheshimiwa Naibu Waziri alitamka mwenyewe kwamba atawapelekea fedha ya kujenga. Kwa kuwa wananchi wameanza kujenga madarasa matatu sasa hivi, ni lini fedha zitakwenda ili kuwasaidia wananchi kujenga Shule ya Sekondari Kurusanga?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari katika kata ambazo hazina shule za sekondari, na katika kata ambazo wanafunzi wamekuwa wengi kuliko kiasi kinachotakiwa kwa kila shule.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mheshimiwa Getere, amefuatilia sana kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo, na pia niwapongeze sana wananchi wa Jimbo la Bunda wakiongozwa na Mheshimiwa Mbunge kwa kuanza ujenzi wa madarasa. Niwahakikishie kwamba katika bajeti zetu tutaweka kipaumbele, kuhakikisha kwamba shule hiyo inapelekewa fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa madarasa na miundombinu mingine. (Makofi)

Name

Edefonce Joackim Canoni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Primary Question

MHE. SHEILA E. LUKUBA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Shule mpya za Sekondari katika Kata za Mawasiliano na Luhungo ili kupunguza msongamano wa wanafunzi?

Supplementary Question 3

MHE. EDIFONSI J. KANONI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza. Ni lini sasa Serikali itajenga sekondari katika Kata ya Sundu katika Jimbo la Kalambo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kanoni, Mbunge wa Jimbo la Kalambo alishaleta taarifa ya kata ambazo hazina shule za sekondari na kata ambazo shule zake zimekuwa na wanafunzi wengi zaidi kwa ajili ya kutenga bajeti ya kwenda kujenga shule hizo.

Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tutafuatilia vigezo vya kata hiyo ili tuweze kuona namna nzuri ya kuanza kutenga bajeti mapema iwezekanavyo kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ya sekondari katika eneo hilo.

Name

Suma Ikenda Fyandomo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SHEILA E. LUKUBA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Shule mpya za Sekondari katika Kata za Mawasiliano na Luhungo ili kupunguza msongamano wa wanafunzi?

Supplementary Question 4

MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa swali dogo la nyongeza. Shule ya Sekondari ya Tukuyu Mjini haina bwalo kwa miaka mingi. Ile shule ni kongwe, ina zaidi ya miaka 20, wanafunzi wanakula wakiwa wamesimama na hali ya hewa ya Tukuyu ni mvua na ni baridi kali. Je, ni lini Serikali itajenga bwalo kwa ajili ya Shule ya Tukuyu Sekondari? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, moja ya vipaumbele ambavyo Serikali imeweka katika sekta ya elimu hususan sekondari, ni kuhakikisha kwamba shule zetu zinakuwa na miundombinu muhimu yakiwemo mabwalo ili kuwawezesha watoto kupata chakula katika mazingira bora, nai pia na shughuli nyingine zinazofanyika katika shule zetu.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Shule ya Sekondari ya Tukuyu haina bwalo, na ninafahamu kwamba tulishatoa maelekezo kwa Wakurugenzi kuwasilisha maombi kwa ajili ya ujenzi wa mabwalo katika shule kama hizo. Kwa hiyo, nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI kumsisitiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kuwasilisha mapema iwezekanavyo maombi ya fedha kwa kadiri ya ramani na BOQ iliyoandaliwa ili tuweze kuona namna ya kuanza kutoa fedha hizo kwa awamu, tuanze kujengwa bwalo hilo ili watoto wetu wasome katika mazuri zaidi.