Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 34 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 400 | 2026-05-21 |
Name
Sheila Edward Lukuba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHEILA E. LUKUBA aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Shule mpya za Sekondari katika Kata za Mawasiliano na Luhungo ili kupunguza msongamano wa wanafunzi?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Sheila Edward Lukuba, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ina kata 29 ambapo kata 28 zina shule za sekondari isipokuwa kata moja ya Luhungo ambayo haina shule ya sekondari kutokana na changamoto ya kupata eneo linalofaa kwa ajili ya ujenzi wa shule.
Mheshimiwa Spika, mwaka 2025/2026 Serikali imetenga shilingi milioni 528.99 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika Mtaa wa Mawasiliano uliopo Kata ya Mkundi ili kupunguza msongamano katika shule ya sekondari ya Mkundi Mlimani iliyopo katika Kata ya Mkundi ambayo kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 2,228. Ujenzi wa shule hii utawapunguza umbali wa kufuata shule, kwa wanafunzi wanaoishi katika Mtaa wa Mawasiliano na maeneo ya jirani.
Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Kata ya Luhungo inapata shule ya sekondari, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imeanza kufanya mazungumzo na uongozi wa Jeshi la Wananchi, Kambi ya Mzinga ili kuona uwezekano wa kupata eneo linalokidhi vigezo kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Luhungo, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved