Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

John Stephano Luhende

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukene

Primary Question

MHE. JOHN S. LUHENDE aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza utekelezaji wa ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami kutoka Nzega – Itobo – Igusule hadi Kagongwa?

Supplementary Question 1

MHE. JOHN S. LUHENDE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia kwamba Serikali kwa sasa ina ujenzi mkubwa wa SGR, wananchi wa Wilaya ya Nzega na Wilaya ya Igunga tunategemea kutumia mradi huo kupitia Barabara hiyo ya Nzega – Itobo hadi Bukene. Je, nini mpango wa Serikali kuhusu ukamilishaji wa barabara hiyo ili tuweze kunufaika na SGR wakati itakapokamilika?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mpango wa Serikali na hasa kwa vituo vyote vya SGR, vituo vyote vimeainishwa ambavyo wananchi watakuwa wanavitumia wakati wa SGR na vimepangiwa bajeti vijengwe, yaani barabara zijengwe kutoka kwa wananchi hadi kwenda kwenye vituo, kuanzia Dar es Salaam mpaka kote Mwanza na mpaka Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, barabara zote zimeainishwa. Kama hiyo itakuwa ni moja ya barabara, basi iko kwenye mpango wa kuijenga ili kuwaunganisha wananchi kwenye barabara kubwa na vituo vya SGR kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachoweza kusema kwa Mheshimiwa Mbunge, kama Bukene ndiyo kituo kikuu ambacho SGR itakuwa na kituo, nitaomba tuonane ili tuweze kujiridhisha kama ni moja ya vituo ambavyo vitajengwa barabara ya lami, ahsante.