Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 29 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 346 2026-05-14

Name

John Stephano Luhende

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukene

Primary Question

MHE. JOHN S. LUHENDE aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza utekelezaji wa ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami kutoka Nzega – Itobo – Igusule hadi Kagongwa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa John Stephano Luhende, Mbunge wa Bukene, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Nzega – Itobo – Igusule hadi Kagongwa, kilometa 65, unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Hadi sasa jumla ya kilometa 18.3 kuanzia Kagongwa hadi Igusule zimejengwa mpaka tabaka la tatu la barabara kwa ufadhili wa mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta (EACOP). Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha ili kumalizia ujenzi wa tabaka la lami kwa sehemu hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sehemu ya barabara hii iliyobaki kuanzia Igusule hadi Nzega, urefu wa kilometa 46.7 itajengwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha, ahsante.