Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Daniel Awack Tlemai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karatu

Primary Question

MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Njiapanda – Mang’ola – Matala, ili wakulima waweze kusafirisha mazao yao kipindi cha masika?

Supplementary Question 1

MHE. DANIEL A. TLEMAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu aliweza kutembelea eneo hilo la Bonde la Eyasi, kutoka Karatu – Njiapanda kwenda Eyasi, pia, Naibu Waziri alikuwepo katika msafara huo na alijionea hali ya barabara hiyo ya kutoka Karatu kwenda Mangolo kilometa 50, je, sasa Serikali ina mkakati gani wa kutafuta fedha ili kuitengeneza kwa kiwango cha lami barabara hiyo yenye kilometa 50, ambayo ni kutoka Njiapanda kwenda Mang’ola?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema katika jibu langu la msingi, moja ni kwamba, barabara hii tumeisanifu yote kutoka Karatu, Mang'ola hadi Matala kwenda Sibiti. Bahati nzuri, kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge, nilikuwepo katika ziara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Serikali, tunatambua kwamba, eneo hili la Mang’ola ndilo linazalisha zao la kitunguu ninadhani Tanzania na kwa Afrika Mashariki nzima. Waziri Mkuu alitoa maelekezo kwamba, hiyo barabara walau tuanze kuijenga kwa awamu kwenda Mang'ola ambako tayari pia kuna skimu kubwa sana ya umwagiliaji. Pamoja na kuanza, hata kama ni kwa awamu, ifike kwenye hospitali ya Wilaya, kilometa tano, ambayo pia ipo katika hiyo barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, maelekezo ya Waziri Mkuu yamezingatiwa, na tumeiweka katika mpango wa kuanza kuijenga, endapo tutakuwa tumepitishiwa bajeti yetu ambayo tunategemea kuiwasilisha katika siku zinazofuata, ahsante.