Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 29 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 345 | 2026-05-14 |
Name
Daniel Awack Tlemai
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Karatu
Primary Question
MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Njiapanda – Mang’ola – Matala, ili wakulima waweze kusafirisha mazao yao kipindi cha masika?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Daniel Awack Tlemai, Mbunge wa Karatu, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali, kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), tayari imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kuijenga barabara hii yote kwa kiwango cha lami. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hiyo, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved