Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Khalid Mussa Nsekela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyerwa
Primary Question
MHE. KHALID M. NSEKELA aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha pembejeo, huduma za ugani, bei na masoko ya uhakika ya Kimataifa kwa zao la kahawa katika Jimbo la Kyerwa?
Supplementary Question 1
MHE. KHALID M. NSEKELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Ninashukuru kwa majibu mazuri kutoka kwa Naibu Waziri. Kwa kuwa, Wilaya ya Kyerwa inaongoza kwa uzalishaji mkubwa wa zao la kahawa, na ni zao ambalo linaongoza kwa kuingiza fedha za kigeni, je, Serikali haioni kwamba, ni muda muafaka sasa kuifanya Kyerwa iwe sehemu ya kipaumbele na kimkakati kwa ajili ya uzalishaji wa zao hili la kahawa?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ninampongeza kaka yangu Khalid Mussa Nsekela, Mbunge wa Kyerwa, kwa swali lake la msingi. Namthibitishia tu kwamba, Kyerwa ni miongoni mwa halmashauri ambazo sisi Wizara ya Kilimo tunaziangalia kwa jicho la karibu. Ndiyo maana utaona katika miaka hii miwili tu ya fedha, tumepeleka miche mingi, na bado tutaongeza, lakini siyo katika halmashauri yake tu, yaani ni katika ule Mkoa mzima wa Kagera. Ni moja ya mikoa ambayo sasa tunafufua kabisa zao la kahawa kwa sababu, ni zao ambalo linatuletea fedha nyingi za kigeni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hilo lipo ndani ya mipango, na tunaendelea kutekeleza kwa kuongeza hizo pembejeo, miche pamoja na Maafisa Ugani katika eneo lake. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved