Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 29 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 344 2026-05-14

Name

Khalid Mussa Nsekela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. KHALID M. NSEKELA aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha pembejeo, huduma za ugani, bei na masoko ya uhakika ya Kimataifa kwa zao la kahawa katika Jimbo la Kyerwa?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Serikali kupitia Bodi ya Kahawa Tanzania inatekeleza mpango wa kuzalisha na kusambaza bure miche bora ya kahawa kwa wakulima, ambapo katika kipindi cha msimu wa mwaka wa fedha 2022/2023 hadi 2024/2025 jumla ya miche 9,406,192 ya kahawa imesambazwa bure kwa wakulima wa Kahawa, Wilayani Kyerwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, Serikali imeimarisha huduma za ugani kwa Wilaya ya Kyerwa kwa kuwapatia Maafisa Ugani pikipiki 33 na mashine moja ya kupimia afya ya udongo. Aidha, jumla ya wakulima 300 wa zao la kahawa wamepatiwa mafunzo kuhusu kilimo bora cha zao la kahawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, Serikali inaendelea kutekeleza Mkakati wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Tasnia ya Kahawa. Lengo la Mkakati huo ni kuimarisha na kuongeza wigo wa mauzo ya kahawa katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza hilo, Serikali imeanza kutumia Balozi za Tanzania nje ya nchi kuitangaza kahawa ya Tanzania kupitia mikutano, makongamano na maonesho ya Kimataifa, ikiwemo Africa Fine Coffee Association Conference and Exhibition, na maonesho makubwa ya kahawa Japan. Jitihada hizi zinalenga kuongeza mauzo ya kahawa yetu katika masoko mapya katika nchi za Algeria, Morocco, China, Korea ya Kusini, Marekani, Canada, Urusi, China, Misri na Japan.