Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Devotha Methew Minja

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DEVOTA M. MINJA K.n.y. MHE. KIZA H. MAYEYE aliuliza: - Je, Serikali imechukua hatua gani za kuchochea viwanda vya kuongeza thamani ya zao la chikichi ili kupunguza uagizaji wa mafuta ya kula nje ya nchi?

Supplementary Question 1

MHE. DEVOTA M. MINJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Waziri amesema Serikali ina mkakati wa kuhakikisha sasa zao la mchikichi linazalishwa katika Mikoa ya Morogoro na Kigoma. Serikali kwa sasa inatumia gharama kubwa sana kuingiza mafuta nchini kwa sababu, hatuna uwezo wa kuzalisha. Iko mikoa mingine mingi ambayo ina uwezo wa kuwa na mazao ya mchikichi mbali na Kigoma na Morogoro. Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha mikoa hiyo na yenyewe inazalisha michikichi, ili tupate mafuta ya kutosheleza nchi?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakiri kwamba, bado tuna changamoto ya uzalishaji wa mafuta nchini, na ndiyo maana moja ya jitihada kubwa ya Serikali sasa ni kuhakikisha kwamba, tunaongeza uzalishaji nchini, na siyo tu kwenye zao la chikichi peke yake, hata alizeti bado tunaweka msisitizo. Kwa hiyo, Wizara imefanya mapping ya kuainisha kila zao linafiti eneo gani. Kwa hiyo, kwa tafiti zilizofanyika sasa, inaonesha chikichi inakubali zaidi katika Mikoa ya Kigoma na Morogoro ambako sasa tunataka tuweke msisitizo mkubwa na maeneo mengine ndiyo tutaweka msisitizo kwenye mazao kama ya alizeti, karanga na ufuta, ambayo yote yanaleta matokeo ya mafuta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, jukumu la Serikali ni kuendelea kufanya tafiti. Tukipata katika hayo maeneo mengine, kama mikoa ambayo anaitaja Mheshimiwa Mbunge, tutafanya hivyo, ili kuhakikisha kwamba chikichi inaenda katika maeneo mengi na uzalishaji unaongezeka. Ahsante sana.