Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 29 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 343 | 2026-05-14 |
Name
Kiza Hussein Mayeye
Sex
Female
Party
CUF
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DEVOTA M. MINJA K.n.y. MHE. KIZA H. MAYEYE aliuliza: -
Je, Serikali imechukua hatua gani za kuchochea viwanda vya kuongeza thamani ya zao la chikichi ili kupunguza uagizaji wa mafuta ya kula nje ya nchi?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Kiza Hussein Mayeye, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukabiliana na upungufu wa mafuta ya kula nchini, Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuhamasisha kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya mafuta, hususani zao la chikichi. Katika kutekeleza hilo, uzalishaji wa chikichi umeongezeka kutoka tani 51,834.42 mwaka wa fedha 2023/2024 hadi tani 74,302.65 mwaka wa fedha 2024/2025. Lengo ni kuhakikisha upatikanaji wa malighafi za viwanda vya kuongeza thamani ya zao la chikichi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi katika mwaka wa fedha 2026/2027 itazalisha na kusambaza miche ya chikichi 2,000,000 katika maeneo ya uzalishaji na kuendelea kuwezesha uchakataji wa zao la chikichi kwa kutoa mashine 18 za kuongeza thamani zao la chikichi kwenye vyama 18 vya wakulima wa zao hilo. Aidha, Serikali itaendelea kuhamasisha kuongezeka kwa uzalishaji wa zao la chikichi kwa kuanzisha mashamba makubwa ya pamoja yenye ukubwa wa hekta 48,000 kwa ajili ya zao la chikichi katika Mikoa ya Kigoma na Morogoro.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved