Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

William Kafiti Kafiti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Primary Question

MHE. KAFITI W. KAFITI aliuliza: - Je, lini Serikali itaandaa Kanuni za Bima za lazima, ili kutekeleza Sheria ya Fedha ya Mwaka 2022 na kuongeza mapato ya Serikali?

Supplementary Question 1

MHE. KAFITI W. KAFITI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniruhusu niulize swali la nyongeza. Kwa kuwa, sekta ya bima nchini ni moja ya taasisi za kifedha zinazoongeza mapato kwenye mfuko wa Serikali, je, nini sasa kauli ya Mheshimiwa Waziri kwamba, kanuni hizi zitakwenda kukamilika? Nini commitment ya Serikali katika hili? Ahsante.

Name

Mshamu Ali Munde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. ENG. MSHAMU A. MUNDE) : Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu kwenye swali la msingi kwamba mchakato huo unaenda kukamilishwa haraka iwezekanavyo, lakini kwa namna ninavyoona ndani ya mwaka huu, siyo mwaka wa fedha, taratibu hizo zitakuwa zimekamilika.