Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 29 | Finance | Wizara ya Fedha | 342 | 2026-05-14 |
Name
William Kafiti Kafiti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Primary Question
MHE. KAFITI W. KAFITI aliuliza: -
Je, lini Serikali itaandaa Kanuni za Bima za lazima, ili kutekeleza Sheria ya Fedha ya Mwaka 2022 na kuongeza mapato ya Serikali?
Name
Mshamu Ali Munde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Liwale
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. ENG. MSHAMU A. MUNDE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Kafiti William Kafiti, Mbunge wa Ilemela, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Sheria ya Fedha Na. 5 ya Mwaka 2022, imefanya marekebisho ya Sheria ya Bima, Sura 394, ili kuongeza wigo wa bima za lazima kwa lengo la kuongeza kinga kwa majanga, ambayo yana madhara makubwa kwa wananchi yanapotokea. Utekelezaji wa marekebisho hayo katika Sheria husika unailazimu Serikali kuandaa kanuni, kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge amesisitiza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekamilisha maandalizi ya Rasimu ya Kanuni za Bima za Lazima. Kwa sasa, zoezi la ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kuhusu rasimu hiyo, linaendelea. Aidha, kwa kuzingatia umuhimu wa suala hili, Serikali imedhamiria kukamilisha mchakato huu mapema iwezekanavyo. Ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved