Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Chief Thomas Mgonto Kitima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ikungi Mashariki

Primary Question

MHE. THOMAS M. KITIMA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha Sheria ya kuanzisha Mamlaka ya Kusimamia Uwekezaji wa Umma nchini?

Supplementary Question 1

MHE. THOMAS M. KITIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza swali moja dogo la nyongeza. Je, Serikali haioni haja ya kufanya mapitio ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, ili kuweza kuipa nguvu ya kusimamia mitaji ya umma; kwa mfano, kuitengenezea bodi yake, kuibadilisha jina na kufafanua majukumu yake vizuri, ili iweze kutekeleza majukumu yake kisawasawa? Ahsante sana.

Name

Mshamu Ali Munde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. ENG. MSHAMU A. MUNDE) K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatia jibu langu la msingi ni kwamba, kwa sasa wataalamu wanaendelea kupitia rasimu ambayo italetwa Bungeni. Muswada huo utakaoletwa Bungeni baada ya kukamilisha mchakato, unahusisha pia uboreshwaji wa Ofisi ya TR (Treasurer Registrar) ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninafahamu Mheshimiwa Kitima ana lengo la kuhakikisha TR anafanya shughuli zake kikamilifu ili sasa mashirika ya umma ambayo anayasimamia yaweze kuleta tija na yasiwe tanuri la fedha za umma, badala yake ziweze kuchangia kwenye pato la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaendelea kusisitiza kwamba, mchakato ule unahusisha maboresho ya Ofisi ya Msajili wa Hazina. Ninaomba kuwasilisha.