Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 29 | Planning and Investment | Ofisi ya Rais: Mipango na Uwekezaji | 341 | 2026-05-14 |
Name
Chief Thomas Mgonto Kitima
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ikungi Mashariki
Primary Question
MHE. THOMAS M. KITIMA aliuliza: -
Je, lini Serikali itakamilisha Sheria ya kuanzisha Mamlaka ya Kusimamia Uwekezaji wa Umma nchini?
Name
Prof. Kitila Alexander Mkumbo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ubungo
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. ENG. MSHAMU A. MUNDE) K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Thomas Mgonto Kitima, Mbunge wa Ikungi Mashariki, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza sana Mheshimiwa Kitima kwa namna anavyowawakilisha wananchi wake. Pia, kwa kuwa, ninajua kwamba Mheshimiwa Kitima ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, ninafahamu jinsi ambavyo amekuwa mahiri kwenye kusimamia shughuli za Kamati ile, na ni shughuli za Kitaifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ofisi yetu, kwa maana ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, tayari imepokea maelekezo kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi kuhusu Muswada wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma. Kwa sasa, vikao vya kitalaamu vya Serikali vinaendelea kupitia rasimu ya muswada huo. Mara baada ya vikao vya kitaalamu kukamilisha kazi hiyo, ofisi yetu itawasilisha rasimu ya muswada huo Bungeni kwa ajili ya hatua nyingine za kibunge kuelekea kuupitisha kuwa sheria. Ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved