Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ritta Enespher Kabati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya Kata ya Kimara na Idete – Kilolo?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza. Ninashukuru kwanza kwa majibu ya Mheshimiwa Waziri. Kwa kuwa, sera ya Serikali ni kujenga vituo vya afya kila kata na ujenzi wa zahanati kila kijiji, lakini Wilaya yetu ya Kilolo zaidi ya kata 15 hazina vituo vya afya na vijiji 61 havina zahanati. Miundobinu ni mibovu, wazazi wanapata shida kwenda kujifungua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, nini mkakati wa Serikali kutoa kipaumbele kwa maeneo haya ya Kilolo ambayo hayapitiki na hayana barabara, yaweze kujengewa vituo vya afya na zahanati katika vijiji?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, wakati ikiwasilisha Randama, kipindi tunapitisha Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, tuliweka bayana kwamba kipaumbele ni kukamilisha maboma ya zahanati zaidi ya 19,000 na kukamilisha vituo vya afya na vile vituo vya afya vya kimkakati ambavyo nimejibu kwenye swali la msingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Dkt. Kabati kwamba Sera ya Serikali ni kujenga zahanati kila kijiji na tayari tumeshajenga zaidi ya zahanati 6,556, na pia tumejenga vituo vya afya 154 na hospitali 194.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa mipango mizuri ya Serikali ya Awamu ya Sita tutaendelea kujenga vituo vya afya na zahanati, na lile lengo la kufikia kwamba wananchi wetu wapate huduma ndani ya kilometa tano tunaendelea kulifanyia kazi ili wananchi wetu wapate huduma hizi. Ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved