Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 29 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 340 2026-05-14

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya Kata ya Kimara na Idete – Kilolo?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Ritta Ernespher Kabati, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imetoa jumla ya shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Idete. Aidha, ujenzi umehusisha jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD), choo cha nje pamoja na kichomeataka. Ujenzi wa OPD umefika hatua ya lenta sawa na 35%.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali kupitia mapato ya ndani ya halmashauri ya Wilaya ya Kilolo imetenga jumla ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la maabara katika Kituo cha Afya Ilula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeweka kipaumbele cha kukamilisha miradi viporo ya vituo vya afya 364 ili viweze kutoa huduma muhimu zikiwemo huduma za dharura za upasuaji kisha itaendelea na ujenzi wa vituo vya afya katika kata za kimkakati zitakazokidhi vigezo. Ninaomba kuwasilisha.