Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

George Natany Malima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga vituo vya afya katika Kata za Kimkakati za Chunyu, Berege, Godegode na Mlembule - Mpwapwa?

Supplementary Question 1

MHE. GEORGE N. MALIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na jibu zuri la Serikali nina swali moja la nyongeza. Tarehe 2/1/2026, Mheshimiwa Waziri Mkuu alifanya ziara katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Jimbo la Mpwapwa katika Kata ya Gulwe. Alikuwa akikagua uharibifu wa miundombinu ya SGR uliosababishwa na mvua nyingi zilizokuwa zinanyesha. Kwa kuzingatia kwamba Kata ya Gulwe ina kituo…

MWENYEKITI: Mheshimiwa, swali.

MHE. GEORGE N. MALIMA: ...ina stesheni ya SGR. Niliomba kijengwe kituo cha afya ili kukabiliana na matukio ya ajali ambayo yanaweza kutokea. Ninamshukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, wataalamu wamefika tumewaonesha eneo la kujenga kituo cha afya. Sasa ninataka kujua, ni lini ujenzi huu utaanza ili watu hawa wa Gulwe na wasafiri wote wawe katika hali nzuri ya usalama? Ahsante.

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Mheshimiwa Waziri Mkuu alifanya ziara katika eneo hili, na pia alitoa maelekezo ambayo Serikali inakusudia katika mwaka huu wa fedha 2026/2027 kuanza ujenzi katika Kituo cha Afya cha Gulwe ambacho kitahudumia wakazi zaidi ya 13,000, pamoja na wale abiria wanaohudumiwa na kituo chetu cha SGR. Ninaomba kuwasilisha.