Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 29 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 339 2026-05-14

Name

George Natany Malima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga vituo vya afya katika Kata za Kimkakati za Chunyu, Berege, Godegode na Mlembule - Mpwapwa?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa George Natany Malima, Mbunge wa Jimbo la Mpwapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kati ya kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 hadi kufikia mwaka 2025/2026 Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 1.19 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali, lakini imetoa shilingi bilioni 3.4, ujenzi wa vituo vya afya na shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya zahanati katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, imewasilisha maombi Hazina ya jumla ya shilingi bilioni 23.5 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya vya kimkakati 94 ambapo Kata ya Chunyu imetengewa shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa miundombinu muhimu katika vituo vya afya 364 kisha kuendelea na ujenzi wa vituo vya kimkakati kadiri vitavyokidhi vigezo. Ninaomba kuwasilisha.