Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mary Daniel Surati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Serengeti
Primary Question
MHE. MARY D. SURATI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha Halmashauri ya Serengeti inapata Service Levy kutokana na shughuli za utalii Wilayani humo?
Supplementary Question 1
MHE. MARY D. SURATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na ninaishukuru Serikali kwa majibu mazuri, lakini mchakato huu umeanza takribani miaka 16 iliyopita. Sisi Watu wa Serengeti kwa mchango ambao tunachangia kwa Taifa, inakuwaje mpaka leo hii hatunufaiki moja kwa moja katika mapato haya? Ninaomba kujua kwa niaba ya wananchi wa Serengeti; ni lini sisi Watu wa Serengeti tutaanza kupata mapato hayo?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nimhakishie Mheshimiwa Surati kwamba tayari Serikali imelifanyia kazi. Miaka hiyo iliyopita hatukuwa na mwongozo wa 60% kwa halmashauri ambako shughuli zinafanyika kwa maana ya Serengeti kwa muktadha huu na 40% kwa Jiji la Arusha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tushaweka mwongozo huo na umeanza kufanya kazi. Ninaomba nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge, katika kipindi cha mwaka wa fedha huu 2025/2026 kuanzia Machi mpaka Julai Halmashauri ya Serengeti imepata takribani shilingi bilioni 1.51 kutokana na ushuru huo unaotokana na shughuli za utalii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, dalili ni njema. Tunafahamu bado kuna kazi ya kufanya. Nimhakikishie kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, tutalifanyia kazi kuhakikisha kwamba changamoto hii inaondoka na Halmashauri ya Serengeti inanufaika na mapato ya utalii.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved