Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Omary Marcus Msigwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Madaba
Primary Question
MHE. OMARY M. MSIGWA aliuliza: - Je, lini Serikali itaongeza Watumishi wa Sekta ya Afya wakiwemo Wataalamu wa Mionzi katika Jimbo la Madaba?
Supplementary Question 1
MHE. OMARY M. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina swali la nyongeza. Je, ni lini utakuwa tayari kuja kuona Vituo vya Afya Mtyangimbole, Lituta na Matetereka katika Halmashauri mpya ya Jimbo la Madaba ambapo kuna upungufu mkubwa wa watumishi sekta ya afya? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kama ambavyo katika ajira za siku 100 za kwanza za uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Halmashauri ya Madaba ilipata watumishi 84 na tunatambua kwamba kuna upungufu mkubwa wa watumishi katika halmashauri hiyo. Kila kibali cha ajira inapotoka tutahakikisha Halmashauri ya Madaba inapewa kipaumbele ili kuongeza watumishi katika vituo vyake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie kwamba nipo tayari kuambatana naye, tutapanga baada ya Bunge hili ili twende Madaba kupitia kwenye vituo hivyo vya afya alivyovitaja pamoja na kuona hali ya utumishi na kuona namna nzuri zaidi ya kuboresha huduma za afya.
Name
Anne Kilango Malecela
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Same Mashariki
Primary Question
MHE. OMARY M. MSIGWA aliuliza: - Je, lini Serikali itaongeza Watumishi wa Sekta ya Afya wakiwemo Wataalamu wa Mionzi katika Jimbo la Madaba?
Supplementary Question 2
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru, Jimbo la Same Mashariki lina vituo vya afya vitatu, ninaishukuru Serikali, lakini vituo vitatu vya afya vyote havina watumishi wa kutosha. Ukiangalia zahanati za jimbo zima, kila zahanati unakuta ina mganga mmoja tu au wawili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisemi Mheshimiwa Waziri aje kwangu, bali ninaomba akaketi ofisini, aangalie vizuri na aone kwamba kuna umuhimu wa kuniletea watumishi. Je, ataniletea watumishi hao lini?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Jimbo la Same Mashariki katika zahanati na vituo vya afya kuna upungufu wa watumishi, lakini Serikali imekuwa kila ikitoa kibali cha ajira tunahakikisha watumishi wanapelekwa Jimbo la Same Mashariki kama ambavyo tumekuwa tukipeleka kwenye majimbo mengine kote nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Anne Kilango Malecela kwamba Serikali inatambua uhitaji wa watumishi, na kila kibali cha ajira kinapojitokeza, tutahakikisha watumishi wanaopelekwa halmashauri hiyo inakuwa ni kipaumbele cha hali ya juu ili kuendelea kupunguza pengo la watumishi na kuendelea kuboresha huduma kwa wananchi wa Jimbo la Same Mashariki.
Name
Abdallah Dadi Chikota
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyamba
Primary Question
MHE. OMARY M. MSIGWA aliuliza: - Je, lini Serikali itaongeza Watumishi wa Sekta ya Afya wakiwemo Wataalamu wa Mionzi katika Jimbo la Madaba?
Supplementary Question 3
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi. Halmashauri ya Mji Nanyamba ina vituo vya kutolea huduma ya afya viwili; Kituo cha Afya Dinyecha na Hospitali ya Mji Nanyamba zenye X-Ray machine, lakini halmashauri hiyo haina mtaalamu wa mionzi hata mmoja. Je, Serikali itapeleka mtumishi huyo haraka ili ikatoe huduma inayokusudiwa?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba tunavyo vituo vya afya ambavyo Serikali kwa kujali afya za wananchi tulinunua mitambo na mashine za X-Ray vikiwemo Vituo vya Afya viwili katika Halmashauri ya Nanyamba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Abdallah Chikota kwamba Serikali inatambua hatuna watumishi wa X-Ray katika halmashauri hiyo, na hivi sasa tumeanzisha utaratibu wa kupeleka watumishi wanaotoka makazini kwenda kwenye vyuo ambavyo vinafundisha short courses za masuala ya X-Ray na hivi sasa tuna watumishi zaidi ya 150 wanaendelea na kozi hizo katika maeneo mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, baada ya kuhitimu wataalamu hao tutahikikisha maeneo yale ambayo ya mashine za X-Ray na wataalamu hawapo, tunapeleka wataalamu ili tuhakikishe kwamba huduma za X-Ray na Ultra Sound na huduma nyinginezo za vipimo zinafanyika vizuri zaidi.
Name
Zuberi Yahya Mfaume
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Morogoro Kusini
Primary Question
MHE. OMARY M. MSIGWA aliuliza: - Je, lini Serikali itaongeza Watumishi wa Sekta ya Afya wakiwemo Wataalamu wa Mionzi katika Jimbo la Madaba?
Supplementary Question 4
MHE. ZUBERI Y. MFAUME: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa hii. Ninapenda kumwuliza Naibu Waziri kwamba ni lini sasa watumishi wa kada ya afya, katika maabara watakuwa wakipandishwa ngazi za madaraja sambamba kama wenzao wa kada ya famasi pamoja na manesi?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma, na kwa taratibu ambazo zimeendelea kutekelezwa kila kada, ina utaratibu wake, kwanza wa madaraja, pia na utaratibu wake wa kupandishwa vyeo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali hii ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka mitano iliyopita imevunja rekodi ya kupandisha madaraja kwa watumishi wa kada zote; madaktari, wauguzi, walimu na watumishi wote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea kuhakikisha kwamba wale wenye sifa na wanaostahili kupandishwa madaraja, wanapandishwa madaraja yao kwa wakati ili kudumisha utumishi bora katika sekta ya afya, na pia katika sekta zote hapa nchini.
Name
Ester Amos Bulaya
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. OMARY M. MSIGWA aliuliza: - Je, lini Serikali itaongeza Watumishi wa Sekta ya Afya wakiwemo Wataalamu wa Mionzi katika Jimbo la Madaba?
Supplementary Question 5
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi nami niulize swali dogo la nyongeza. Halmashauri ya Mji wa Bunda ina mahitaji ya watumishi kwenye sekta ya afya 854. Waliopo ni 384, upungufu 470 wakiwepo watano kwa ajili ya mionzi. Ni lini sasa Serikali itatupatia wataalamu hawa ili wananchi wangu wawe na uhakika wa kupata huduma nzuri ya afya?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Ester Bulaya kwamba Serikali inatambua kuna upungufu wa watumishi katika vituo vyake vya huduma katika Jimbo la Bunda Mjini, na upungufu huu umetokana na sababu kubwa mbili. Sababu ya kwanza, ni kwa sababu Serikali imejenga vituo vya afya, zahanati na hosptali za wilaya kwa wingi ndani ya miaka mitano. Kwa hiyo, automatically imeleta mahitaji makubwa zaidi ya watumishi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, tunafahamu safari ni hatua, tumeanza kwa kujenga, kupeleka vifaa tiba na sasa tunakwenda kupeleka watumishi kama ambavyo watumishi 5,000 wameajiriwa miezi miwili iliyopita na tutaendela kuhakikisha kwamba tunapeleka watumishi katika Halmashauri ya Bunda Mjini na wataalamu wa X-Ray.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, wapo kwenye mafunzo, tunaendelea kuwapeleka kwa awamu na tutahakikisha maeneo yote yenye mitambo ya X-Ray, Ultrasound na mitambo mingine tunapata wataalamu ili vipimo kwa wagonjwa wetu viwe bora na uhakika zaidi.