Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Thomas Maganga Kampala
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Katavi
Primary Question
MHE. THOMAS K. MAGANGA K.n.y. MHE. SALUM K. SALUM aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Soko la Mnada wa Mifugo ili kuwa na Soko lenye hadhi na kuongeza mapato ya Halmashauri katika Jimbo la Meatu?
Supplementary Question 1
MHE. THOMAS K. MAGANGA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Ninamshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Je, ni lini sasa Serikali itapeleka Mizani kwenye minada hiyo ili kuwasaidia wakulima kuuza mifugo yao kwa kilo kuliko inavyokisiwa kwa sasa? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ni utaratibu wa Serikali, na kwa mujibu sheria, mauzo ya mifugo yanatakiwa kufanyika kwa kufuata taratibu za kuwa na mizani ya kupima uzito wa mifugo hiyo. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa kushirikiana na Wizara husika, Viwanda na Biashara, na Wizara ya Mifugo, tutahakikisha Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, tunawasiliana na kuweka utaratibu wa pamoja ili kuhakikisha kwamba eneo la minada hii linakuwa na mizani kwa ajili ya kupimia mizigo na biashara iende vizuri zaidi.
Name
Dr. Christina Christopher Mnzava
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. THOMAS K. MAGANGA K.n.y. MHE. SALUM K. SALUM aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Soko la Mnada wa Mifugo ili kuwa na Soko lenye hadhi na kuongeza mapato ya Halmashauri katika Jimbo la Meatu?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Mnada wa Tinde ulioko katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ni mnada ambao uko barabarani njia kuu ya kwenda Burundi, Rwanda pamoja na Uganda na hauna uzio. Nini mkakati wa Serikali kutuwekea uzio katika ule Mnada wa Tinde kupunguza ajali?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ninakubaliana na Mheshimiwa Dkt. Christina kwamba Mnada wa Tinde ni mnada mkubwa na unahudumia wafanyabiashara wengi na uko kwenye barabara kuu. Kwa kweli tunahitaji kuwa na uzio ili kwanza kuboresha usalama, lakini pia kuboresha huduma za mnada huo.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nichukue nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI nimwelekeze Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga waanze kutenga fedha za mapato ya ndani ya halmashauri kwa awamu kuanza ujenzi wa uzio huo kwa hatua, wakati Serikali Kuu pia ikiangalia namna nzuri ya kupata fedha na kuweza kuunga mkono juhudi hizo ili mnada ule uboreshwe kuwa wa kisasa zaidi.
Name
Asia Abdulkarim Halamga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. THOMAS K. MAGANGA K.n.y. MHE. SALUM K. SALUM aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Soko la Mnada wa Mifugo ili kuwa na Soko lenye hadhi na kuongeza mapato ya Halmashauri katika Jimbo la Meatu?
Supplementary Question 3
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Je, ni lini Serikali itaboresha ujenzi wa Mnada wa Kateshi?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, mipango ya Serikali ni kwamba maeneo yote yenye uhitaji wa shughuli za kiuchumi na za kijamii yakiwemo masoko, stendi na minada, ni kipaumbele katika mipango ya halmashauri, lakini pia ni kipaumbele katika mipango ya Serikali Kuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Asia Halamga kwamba hoja hiyo tumeichukua, lakini nasisitiza pia kupitia Halmashauri ya Hanang, Mkurugenzi aanze kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya kuanza kuboresha mnada huo wakati Serikali inaendelea na hatua zinazotakiwa.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved