Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Regina Christopher Malima
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. REGINA C. MALIMA aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani mahususi wa muda mfupi na wa kati wa kupunguza changamoto ya ajira kwa Vijana hususan Wahitimu wa Vyuo Vikuu?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. REGINA C. MALIMA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa majibu ya Serikali na ninatambua namna ambavyo Serikali imeendelea kuwekeza katika elimu ya juu hasa vyuo na vyuo vikuu. Ninaipongeza sana Serikali kwa hatua hiyo na ninashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri na nitakuwa na swali moja dogo tu la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, ninataka kujua, je, ni sekta zipi zimepewa kipaumbele katika mipango hiyo ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri ameisema hapa?
Name
Ummy Hamisi Nderiananga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, URATIBU NA WENYE ULEMAVU K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA MAHUSIANO: Mheshimiwa Spika, ninaendelea kumpongeza Mheshimiwa Regina kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya. Kama nilivyojibu kwenye swali la msingi, lakini mtakumbuka tangu Mheshimiwa Rais ameingia madarakani ukiacha siku 100 za Mheshimiwa Rais ambapo tulitoa ajira 12,000 mpaka kufikia mwezi huu wa nne tarehe 11 Serikali imeshaajiri vijana 25,238.
Mheshimiwa Spika, kipaumbele kikubwa cha Serikali tumepeleka vijana kwenye maeneo ya afya na elimu ambapo kulikuwa kuna pengo kubwa la watumishi, na tunaendelea kufanya hivyo kwenye sekta nyingine.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved