Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 16 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano 179 2026-04-24

Name

Dr. Regina Christopher Malima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. REGINA C. MALIMA aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani mahususi wa muda mfupi na wa kati wa kupunguza changamoto ya ajira kwa Vijana hususan Wahitimu wa Vyuo Vikuu?

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, URATIBU NA WENYE ULEMAVU K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA MAHUSIANO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutekeleza mikakati ya kuwawezesha vijana, hususan wahitimu wa vyuo vikuu, ili kupunguza tatizo la ajira. Miongoni mwa hatua hizo ni kuandaa Mwongozo wa Taifa wa Mafunzo ya Uzoefu Kazini wa Mwaka 2017 unaoratibu utoaji wa mafunzo kwa kushirikisha sekta ya umma na binafsi, pamoja na kutekeleza programu ya mafunzo kwa vitendo mahali pa kazi inayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano.

Mheshimiwa Spika, kupitia programu hiyo, jumla ya wahitimu 32,194 wamenufaika kwa kupata ujuzi, maadili ya kazi na uzoefu unaowawezesha kuajiriwa au kujiajiri.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Serikali imeanzisha programu maalum za kuwawezesha vijana katika sekta zenye ajira nyingi kama kilimo (BBT), madini (MBT) na uvuvi (BBT-LIFE), sambamba na kuunganisha Watanzania na fursa za ajira nje ya nchi kupitia mikataba na Qatar, Saudi Arabia, UAE na Iran, ambapo vijana 6,559 wamenufaika kati ya Julai, 2025 hadi Machi, 2026.

Mheshimiwa Spika, vilevile, mikopo yenye masharti nafuu imeendelea kutolewa. Mwaka 2024/2025 shilingi bilioni 36.64 zilitolewa kwa vikundi 2,827, na mwaka 2025/2026 zimetengwa shilingi bilioni 200 kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.