Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Omar Issa Kombo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wingwi
Primary Question
MHE. OMARI ISSA KOMBO aliuliza: - Je, Serikali imefikia hatua gani ya kuanza ujenzi wa Ofisi ya NIDA katika Makao Makuu ya Wilaya ya Micheweni?
Supplementary Question 1
MHE. OMAR ISSA KOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, ninampongeza mtu bingwa sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri, lakini ninaomba kuulizwa maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa siku ya tarehe 31 Januari, 2023 nilihoji juu ya ujenzi wa ofisi hii na Serikali ikatuahidi kwamba imetenga zaidi ya shilingi bilioni 197.9 katika ujenzi wa ofisi mbalimbali, sasa Mheshimiwa Naibu Waziri naomba aniambie, je, ni kiasi gani cha fedha kimetengwa katika Wilaya yetu ya Micheweni kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hii?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Ninaomba kumwuliza Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba Wilaya ya Micheweni ni wilaya ambayo imepelekewa miradi mingi ya maendeleo na Mheshimiwa Dkt. Samia pamoja na Mheshimiwa Dkt. Mwinyi. Kwa kuwa wilaya hii inaendelea kukua, je, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa ofisi hii, Serikali iko tayari kutujengea nyumba za watumishi katika ofisi ya Wilaya ya Micheweni?
Name
Mohammed Mahmoud Ayoub
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chaani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru sana Mheshimiwa Omar Issa Kombo kwa maswali yake mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, ameuliza ni kiasi gani kimetengwa, na alitoa takwimu ya zaidi ya shilingi bilioni 154 zimetengwa kwa alivyopewa taarifa kwa wakati huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli fedha zilitengwa, lakini zilitolewa awamu kwa awamu. Kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ni shilingi bilioni 33 zilitengwa kwa ujenzi kwa ujumla na mwaka wa fedha ujao tutatoa tathmini ya fedha zilizotengwa kwa sababu ujenzi huo hautakuwa wa mwaka mmoja, na hapo nitaweza kutoa tathmini ya kituo kwa kituo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema tu kwamba kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 33, Kituo cha NIDA katika la jimbo lake eneo la Micheweni kitakuwepo. Kwa hiyo, ninamtoa hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba kwenye hilo, na fedha tayari zipo, ndiyo maana tukawa tumetangaza zabuni kwa ajili ya ununuzi wa mkandarasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa nyumba za watumishi, naomba tu kumwarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaendelea kujenga nyumba za watumishi kadri ya hali ya kifedha itakavyoruhusu ambapo kwa sasa tunaanza kukamilisha ujenzi wa Ofisi za NIDA kila wilaya. Halafu hatua ya pili tutakwenda kwenye kuona makazi sasa ya watumishi nayo tunaendelea na utaratibu gani?
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Name
Khalid Mussa Nsekela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyerwa
Primary Question
MHE. OMARI ISSA KOMBO aliuliza: - Je, Serikali imefikia hatua gani ya kuanza ujenzi wa Ofisi ya NIDA katika Makao Makuu ya Wilaya ya Micheweni?
Supplementary Question 2
MHE. KHALID M. NSEKELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Ni upi mpango na mkakati wa Serikali wa kuongeza kasi ya upatikanaji wa vitambulisho vya NIDA kwa wananchi wa Jimbo la Kyerwa?
Name
Mohammed Mahmoud Ayoub
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chaani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru sana Mheshimiwa Khalid Nsekela, Mbunge wa Kyerwa kwa swali lake la msingi na namna anavyowapambania wananchi wa Kyerwa kuweza kupata huduma ya vitambulisho vya NIDA kwa wakati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia NIDA ina mpango mkakati wa kuhakikisha kwamba inawafikia wananchi katika ngazi ya kata ingawa kimuundo NIDA ipo katika ngazi ya wilaya, lakini kwa sasa tuna mpango wa kuwafikia wananchi katika ngazi ya kata.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Jimbo lake la Kyerwa, nataka kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba wiki ijayo watumishi wa NIDA watakwenda Kyerwa kwa ajili ya kuwapatia wananchi wa eneo hilo vitambulisho vya NIDA.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved