Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jamal Ramadhan Mwinyi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bumbwini
Primary Question
MHE. MWINYI JAMAL RAMADHAN aliuliza: - Je, ni wanyama gani wana vibali vya kuwindwa kwa matumizi ya kijamii kwa kuwa nchi yetu ina wanyama wengi katika mapori ya vijijini?
Supplementary Question 1
MHE. MWINYI JAMAL RAMADHAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Ninashukuru kwa kunipa heshima hii kwa kuuliza swali la nyongeza. Kwanza ninamshukuru sana Naibu Waziri kwa majibu mazuri ya Serikali yenye mpango mzuri wa kuwasaidia wananchi kuendelea kutumia maliasili za nchi yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu hayo, ninaomba kumwuliza maswali mawili ya nyongeza. Je, ni taaluma gani iliyoweza kutolewa kwa wananchi ili kuhifadhi zaidi wanyama hawa waliotajwa wasitoweke kwa sababu wana taratibu zao za kuzaa? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kumekuwa na sheria ya kulinda wanyamapori hawa. Serikali haioni kwamba sheria hizi ambazo na wananchi wanazilalamikia, (wanyama wale ambao wanaudhi, na wananchi wanalalamika juu ya mazao yao ikiwemo tembo, simba na Nyati) sasa umefika wakati Serikali kutoa maelekezo maalum kwa wananchi juu ya utaratibu maalum wa kisheria kuhusu yale malalamiko ambayo yanatolewa hasa kwa fidia, malalamiko juu ya wanyama hawa wanaoharibu mazao? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza Mheshimiwa Mwinyi Jamal Ramadhan kwa swali lake zuri la msingi. Ninamwambia tu kwamba, moja, Serikali imekuwa na jitihada kubwa. Kwanza, ni kulinda hawa wanyama wote hatari na hawa wanyama ambao wamekuwa wakitumika kwa ajili ya matumizi ya binadamu na kuna kanuni zake juu ya kuwalinda hawa wanyama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile, panapotokea eneo limekuwa na shida, Wizara imekuwa ikitumia TAWA; yaani kama kuna eneo limevamiwa na tembo, utaona kabisa kunakuwa na operesheni maalum za kwenda kuwaondoa tembo katika eneo husika na kuwarudisha katika maeneo yao. Vilevile, katika maeneo hatarishi, TAWA wamekuwa wakifika katika hayo maeneo na kuangalia ni namna gani ambavyo wanaweza kuvuna wale wanyama, kama kuna maeneo wana mamba wamekuwa wakiwavuna na kuwahamishia katika maeneo mengine ambayo hayana watu wengi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kumekuwa na jitihada kubwa zikiwemo kutoa taarifa kupitia vyombo vya habari, wamekuwa wakielimisha. Pia wamekuwa wakifanya mikutano ya hadhara katika maeneo ambayo yamekuwa na hatari zaidi ya kukutana na hawa wanyama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, bado Serikali inafanya kazi nzuri kuhakikisha kwamba hakuna athari kubwa kwa wananchi, lakini wakati huo huo tumehakikisha tunaendelea kuwalinda hawa wanyama kwa faida ya Taifa letu na wananchi katika maeneo husika. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved