Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Morris Joseph Makoi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Mjini
Primary Question
MHE. MORRIS J. MAKOI aliuliza: - Je, lini Serikali itamrejesha mkandarasi wa barabara ya Moshi International School - Kibosho kwa Rafael yenye urefu wa kilometa 5.49?
Supplementary Question 1
MHE. MORRIS J. MAKOI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Kwa sababu sasa tangu Serikali ilipokubali kumleta mkandarasi kufanya kazi hiyo, ni mwaka wa pili sasa; na kwa vile wananchi ambao waliruhusu maeneo yao barabara ipite waliharibu mazao yao na wengine nyumba zao zilivunjwa wakitarajia kwamba barabara ya lami itajengwa na watanufaika na uwepo wa barabara; na kwa vile mpaka sasa hivi hakuna kinachoendelea na mkandarasi hayupo, je, Serikali iko tayari kuwalipa fidia wananchi wale kwa mazao yao na nyumba zao zilizovunjwa ili itakapojengwa barabara wawe hawakuathirika? Hilo ni swali la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; katika barabara hiyo iko barabara ya mchepuko ambayo inaenda kwa wawekezaji; mmoja wa mashamba ya maua na mmoja anajenga hospitali ya kitalii ya shilingi bilioni 17. Daraja limekatika na mpaka tunapoongea hakuna mawasiliano. Je, Serikali iko tayari kutumia fedha za dharura ambazo zimetengwa kutokana na hali ya mafuriko na mvua nyingi zilizotokea kurejesha daraja lile ili kuwarejeshea wawekezaji wale moyo wa kuendelea na kazi ya uzalishaji maua pamoja na ujenzi wa hospitali hiyo? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Makoi, pamoja na wananchi wa Moshi Vijijini kwamba ni dhamira ya dhati ya Serikali kuijenga hiyo barabara kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge ameeleza mara kadhaa kwamba tuna miradi ambayo tulikuwa tumesaini na mingine imeanza, lakini tukawa tumechelewa kulipa advance ama hati zile za awali za malipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba hao wananchi wasiwe na wasiwasi. Sisi kama tulivyosema kwenye jibu letu la msingi, tunaamini kwamba muda siyo mrefu tutamlipa huyu mkandarasi malipo yake ya awali ili aweze kurejea na kuanza kufanya hiyo kazi kama ambavyo tumekubaliana kwenye mkataba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili, barabara aliyoisema ni barabara ambayo inahudumiwa na wenzetu wa TARURA na hata hizi barabara nyingi ambazo tumezifanya tumekuwa tukisaidiana na wenzetu wa TARURA. Tumelipokea hilo kuhusu daraja lilivyovunjika na ninaomba nitumie nafasi hii pia kumwelekeza Meneja wa Mkoa wa Kilimanjaro wakisaidiana na meneja mwenzake wa TARURA Mkoa wa Kilimanjaro waweze kufika eneo hilo ili waone namna watakavyofanya kulijenga hilo daraja na kurejesha mawasiliano ambayo yamekatika. (Makofi)
Name
Dr. Wilson Charles Mahera
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Primary Question
MHE. MORRIS J. MAKOI aliuliza: - Je, lini Serikali itamrejesha mkandarasi wa barabara ya Moshi International School - Kibosho kwa Rafael yenye urefu wa kilometa 5.49?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. WILSON C. MAHERA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Barabara ya Busegwe – Kitaramanka ya kilometa 38.5 ambayo inapita katika kata tano za Jimbo la Butiama ni barabara muhimu sana. Barabara hii Mheshimiwa Rais alituahidi kwamba itapata lami. Sasa ningependa kujua Serikali imefikia hatua gani katika maandalizi ya kuifanya ipate lami?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba ahadi za viongozi wa Kitaifa na hasa Mheshimiwa Rais huwa ni maelekezo. Sisi kama Wizara, baada ya kupata hayo maombi tumeshaanza kufanya taratibu. Ninamwomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira, bajeti yetu bado haijapitishwa, kwa hiyo, tuna hakika itakuwa kwenye utaratibu wa kufanya mipango ya kuanza kuijenga kama ambavyo Mheshimiwa Rais alitoa hiyo ahadi kwa wananchi.
Name
Enock Zadock Koola
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vunjo
Primary Question
MHE. MORRIS J. MAKOI aliuliza: - Je, lini Serikali itamrejesha mkandarasi wa barabara ya Moshi International School - Kibosho kwa Rafael yenye urefu wa kilometa 5.49?
Supplementary Question 3
MHE. ENOCK Z. KOOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona. Barabara kongwe ya Pofo – Mandaka – Kilema ya kilometa 7.2 ilikuwa ahadi ya Mheshimiwa Rais, lakini pia Waziri Mkuu. Sasa barabara hiyo ina hali mbaya sana. Je, ni lini Serikali itaenda kukamilisha ujenzi wa hiyo barabara? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli hii barabara pia ni mojawapo ya barabara ambazo zimekasimiwa kwetu kutoka TARURA, na tumekuwa tunaendelea kuzijenga kwa awamu kwa kiwango cha lami. Ninataka nimhakikishie pia Mheshimiwa Mbunge kwamba hata katika bajeti hii ambayo tunaiendea, tumeiweka katika utaratibu wa kuendelea kuijenga kwa awamu kwa kiwango cha lami.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved