Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ester Amos Bulaya
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: - Je, lini Serikali itatimiza ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mtitaa Bahi?
Supplementary Question 1
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niulize maswali mawili madogo ya nyongeza. Katika Jimbo la Bunda Mjini kuna Kituo cha Afya cha Bunda Mjini na kinatoa huduma ya afya kwa watu wengi sana kuliko vituo vingine vya afya vyovyote takribani kwenye zile kata saba za Bunda Mjini. Hata hivyo, kuna changamoto ya OPD ambapo inahitajika shilingi milioni 182; kuna changamoto ya wodi ya wanawake, wanaume na watoto ambayo ukijumlisha zote gharama yake inayohitajika ni shilingi milioni 695.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini sasa Serikali itatoa fedha ili wananchi wa Jimbo la Bunda Mjini na wa Kata ya Bunda Mjini waweze kupata huduma safi za afya?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kama ambavyo kilivyo Kituo cha Afya cha Mtitaa kwa Mheshimiwa Nollo, ndiyo hivyo hivyo Kituo cha Afya cha Manyamanyama, ni cha muda mrefu; na Mheshimiwa Waziri anakijua. Aidha, Manyamanyama ndiyo kata ninayotoka mimi Mbunge na Mbunge wa Afrika Mashariki. Je, ni lini mtakikarabati Kituo hicho cha Afya cha Kata ya Manyamanyama?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimthibitishie dada yangu Mheshimiwa Ester Bulaya, kwamba tunatambua kwamba Kituo cha Afya cha Bunda Mjini ni kituo ambacho kwa kweli kinahudumia wananchi wengi, wajawazito na wagonjwa wa magonjwa mbalimbali, na ni kituo tegemezi sana kwa wananchi wa Bunda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimeshafanya ziara pale miaka miwili au mitatu iliyopita, na tulikubaliana kwamba Halmashauri walete andiko la mapendekezo. Ninaomba nimhakikishie kwamba walishawasilisha na kimeingizwa kwenye mpango wa vituo ambavyo vina upungufu wa miundombinu. Tutatafuta fedha kwenda kujenga OPD, kujenga wodi na baadhi ya miundombinu ambayo Mheshimiwa Mbunge taarifa zake tunazo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie yeye na wananchi wote wa Jimbo la Bunda Mjini kwamba Serikali hii iko kazini. Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, daktari namba moja anajali afya za wananchi wa Bunda na tutahakikisha tunapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hiki cha afya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, vipo vituo vya afya kongwe na chakavu, na Serikali ilishavitambua vituo vya afya 205 ambavyo ni vya miaka mingi na vinahitaji ukarabati na mara nyingine ujenzi kabisa, kikiwemo Kituo cha Afya cha Manyamanyama, ambako Mheshimiwa Mbunge anatoka na Mbunge wa Afrika Mashariki anatoka. Nimhakikishie kwamba mpango huu tutakwenda kuutekeleza kwa awamu kuhakikisha kwamba vituo vyote chakavu, hospitali na zahanati chakavu zinakwenda kukarabatiwa kwa awamu.
Name
George Natany Malima
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpwapwa
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: - Je, lini Serikali itatimiza ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mtitaa Bahi?
Supplementary Question 2
MHE. GEORGE N. MALIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi. Je, ni lini Serikali itajenga vituo vya afya kwenye kata za kimkakati; Kata ya Godegode, Berege na Chunyu zilizopo katika Jimbo la Mpwapwa?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Malima alishawasilisha orodha ya kata za kimkakati. Serikali inaendelea na taratibu za kupata fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vituo hivyo vya afya.
Name
Sikudhani Yasini Chikambo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: - Je, lini Serikali itatimiza ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mtitaa Bahi?
Supplementary Question 3
MHE. SIKUDHANI Y. CHIKAMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Afya cha Nampungu ni miongoni mwa vituo vya afya vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru. Kituo kile ni kipya, kilitengewa shilingi milioni 500, zimepelekwa shilingi milioni 250 na kwa sasa kituo kimesimama, hakuna ujenzi unaoendelea. Je, Serikali ina kauli gani katika kuhakikisha kwamba tunapeleka fedha ili ujenzi ukamilike? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ni kweli kwamba viko vituo vya afya ambavyo vilipelekewa fedha kwa awamu mbili; shilingi milioni 500 na shilingi milioni 250. Viko ambavyo vimekamilika vimeanza kutoa huduma na vipo ambavyo bado havijakamilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kauli ya Serikali ni kwamba, kwanza Wakurugenzi wa Halmashauri kote nchini ambao walipokea fedha na kujenga vituo vya afya ambavyo havijakamilika, moja wawasilishe taarifa hiyo Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, watenge fedha za mapato ya ndani kwa uwezo wao angalau kukamilisha maeneo ambayo wanaweza kukamilisha ili angalau huduma za wagonjwa wa nje (OPD) zianze kwenye vituo hivyo wakati tunaendelea na hatua za ukamilishaji wa miundombinu iliyosalia.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved