Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 24 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 269 2026-05-07

Name

Kenneth Ernest Nollo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bahi

Primary Question

MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: -

Je, lini Serikali itatimiza ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mtitaa Bahi?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Kenneth Esnest Nollo, Mbunge wa Jimbo la Bahi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Afya Mtitaa kilichopo katika Kata ya Mtitaa Halmashauri ya Bahi ni miongoni mwa vituo vya afya kongwe 205 ambavyo Serikali imevianzisha kwa ajili ya ukarabati na kuviongezea miundombinu ili viweze kutoa huduma ya afya ngazi ya kituo cha afya, ikiwemo huduma ya upasuaji wa dharura kwa wajawazito.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali kupitia Mradi wa Benki ya Dunia wa Usafi na Afya ya Mazingira (WASH) ilitoa shilingi milioni 73.83 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya majisafi na majitaka pamoja na ujenzi wa choo cha nje kwa ajili ya wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Mtitaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya vituo vya afya kongwe kote nchini. Aidha, katika mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali imetenga shilingi milioni 130 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Babayu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi.