Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Joseph Zacharius Kamonga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ludewa
Primary Question
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: - Je, lini Vijiji vya Kitewele, Kimata, Ndoa, Chanjale, Nkanda, Lumbila, Nsele na Kilondo vitawashiwa umeme?
Supplementary Question 1
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Awali ya yote nitumie nafasi hii kuishukuru sana Serikali kwa kutuletea gari ya kubebea nguzo ile yenye winch. Kwa muda mrefu tulikuwa tunasubiri nguzo moja ikidondoka, gari itoke Makete. Kwa hiyo, sasa hivi tuna gari yetu, tunaishukuru sana Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na shukrani hizo, nina maswali madogo mawili ya nyongeza. Mosi, kwa kuwa mradi huu wa vijiji vya ziwani ni mkubwa, na ninakiri kwamba wananchi wanaridhika na kasi ya jeshi, SUMA JKT, je, Serikali haioni haja ya kumwelekeza mkandarasi aongeze kikosi kingine cha pili ambacho labda kianzie huku maeneo ya Kitewele ili wakakutane katikati?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ninatambua kwamba Serikali ilitenga shilingi bilioni sita kwa ajili ya kurekebisha miundombinu ya umeme kwenye vijiji 20 vilivyokuwa vinahudumiwa na mwekezaji binafsi, kampuni ya Madope. Je, kwa kuwa fedha hizi zimeshatoka, ni lini Serikali itatuma wataalam kule Ludewa waanze kazi ya kurekebisha miundombinu hii?
Name
Salome Wycliffe Makamba
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Kwanza kabisa, ninampongeza ndugu yangu Mheshimiwa Kamonga kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwapambania wananchi wake wa Jimbo la Ludewa. Alipambana sana katika kuhakikisha kwamba miundombinu ya usambazaji wa umeme katika jimbo lake inaimarishwa kwa sababu ilikuwa inasuasua, na ni kikwazo kikubwa sana cha Uchumi. Ninampongeza sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye swali lake la kwanza, ni kweli kwamba mkandarasi Suma JKT analo takwa la kimkataba kuhakikisha kwamba anamaliza mradi huu ndani ya wakati. Nitumie fursa hii kuwaagiza REA wamsimamie mkandarasi huyu atimize majukumu yake, apeleke timu ya kutosha na vifaa vya kutosha kuhakikisha wananchi wa Ludewa wananufaika na uwepo wa nishati imara na ya uhakika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili, hili nalo ninampongeza Mheshimiwa Mbunge, alipambana sana kuhakikisha fedha inapelekwa. Hadi sasa hivi tumeshapata shilingi bilioni sita ambazo zinakwenda kutekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu mipya ya usambazaji wa umeme.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ajili ya hili, ndani ya mwezi huu niwaelekeze REA waende wakakae na kuona ni namna gani utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu mipya kwa shilingi bilioni sita ambayo tayari Serikali imeshapeleka unaanza kutekelezwa mara moja. Tunaendelea kutafuta fedha nyingine ili kuhakikisha kwamba utakamilika ndani ya mwaka huu wa fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana.
Name
Joseph Enock Tama
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kaliua
Primary Question
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: - Je, lini Vijiji vya Kitewele, Kimata, Ndoa, Chanjale, Nkanda, Lumbila, Nsele na Kilondo vitawashiwa umeme?
Supplementary Question 2
MHE. JOSEPH E. TAMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza swali. Pamoja na kazi nzuri wanazofanya Wizara ya Nishati, ninaomba kuuliza swali dogo la nyongeza. Ni lini Serikali itawasha umeme kwenye vijiji vya Nsimbo, Mpongolwe, Isunda, Luyembe na Sentaelo katika Jimbo la Kaliua?
Name
Salome Wycliffe Makamba
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyosema Mheshimiwa Rais kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge letu, hadi sasa vijiji vyote ndani ya nchi yetu vimeshapata umeme.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge wa Kaliua, kaka yangu, kwa kweli safari hii Kaliua wametuletea Mbunge wa moto sana. Yuko mbio kuhakikisha anapata matokeo. Hii ni kwa sababu tangu ameingia Bungeni mpaka sasa hivi tumefanikiwa kumpelekea vitongoji 22 ambavyo wakandarasi wako site kwa ajili ya kufanya survey na kupeleka umeme.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, ndani ya mwaka huu wa fedha vitongoji 22 ambavyo tumepeleka, na hivi alivyovitaja, vimo ndani yake vitapatiwa umeme, na hili kwake Mheshimiwa Mbunge tutakwenda kuwasha pamoja vitongoji, ahsante.
Name
Edward Olelekaita Kisau
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kiteto
Primary Question
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: - Je, lini Vijiji vya Kitewele, Kimata, Ndoa, Chanjale, Nkanda, Lumbila, Nsele na Kilondo vitawashiwa umeme?
Supplementary Question 3
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa nafasi. Kijiji cha Enguserosidani tumepata wafadhili wanaotuchimbia maji. Kikwazo tu ni umeme na ni shilingi milioni 140. Je, Wizara hii ina kauli gani kuhusu wawekezaji hawa wanaotaka kuwapa Watanzania hao maji?
Name
Salome Wycliffe Makamba
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Ninakushukuru. Pia ninampongeza Mheshimiwa Edward Olelekaita kwa kupambania wananchi wake wa Kiteto. Bahati nzuri Kijiji hicho anachokisema tulishawahi kwenda tukala nyama ya mbuzi pale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania wa Kiteto wanatudai Wizara ya Nishati kuhakikisha miundombinu yote ya Serikali inayojengwa, siyo tu kisima, hata shule, vituo vya afya na zahanati vinapelekewa nishati ya umeme ili kuongeza tija na kufungamanisha miradi ya Serikali ili iweze kuleta manufaa kwa wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye eneo hili la maji niwaelekeze watu wa REA walioko katika kijiji hiki kuhakikisha wanafikiwa na miundombinu ya umeme ili kisima hiki kiwanufaishe Wanakiteto.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved