Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
1961-1995 Session 1 Sitting 1 Energy and Minerals Wizara ya Nishat 121 2026-04-17

Name

Joseph Zacharius Kamonga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ludewa

Primary Question

MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: -

Je, lini Vijiji vya Kitewele, Kimata, Ndoa, Chanjale, Nkanda, Lumbila, Nsele na Kilondo vitawashiwa umeme?

Name

Salome Wycliffe Makamba

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Zacharius Kamonga, Mbunge wa Ludewa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua kwamba baadhi ya kaya katika vijiji hivi vilivyotajwa zinatumia umeme wa nguvu ya jua (solar). Hata hivyo, Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika, imetenga kiasi cha shilingi bilioni 3.21 kupitia REA kwa ajili ya kusambaza umeme katika vitongoji vilivyopo ndani ya Vijiji tisa vya Kitewele, Kimata, Ndoa, Chanjale, Kanda, Uzila, Mstele na Kilondo Mkoani Njombe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambua changamoto ya jiografia na ugumu wa kufikisha vifaa katika maeneo hayo, tumempatia kazi hiyo mkandarasi SUMA JKT Electric Company Limited ambaye tumemwelekeza kufanya kazi kwa nguvu zote kama jeshi, na kuhakikisha kuwa azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kufungamanisha nishati na maendeleo ya kiuchumi inatimia. Mradi huu unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba, 2026.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.