Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Arif Suleiman Premji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtwara Vijijini

Primary Question

MHE. ARIF S. PREMJI aliuliza:- Je, Shule ngapi za kidato cha tano na sita zimejengwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 hadi kufikia robo ya pili?

Supplementary Question 1

MHE. ARIF S. PREMJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Jimbo la Mtwara Vijijini lina kata 21. Katika kata hizo, ni shule moja tu ndiyo ina kidato cha tano na sita. Je, ni upi mkakati wa Serikali kuhusiana na hilo ili kuongeza shule za sekondari katika Jimbo la Mtwara Vijijini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, wanafunzi 756 ndio wapo kwenye shule ya Mustafa Sabodo High School. Shule hiyo inapitia changamoto ya uzio. Ipi kauli ya Serikali kuhusiana na changamoto hiyo na ambavyo wanaweza wakaitatua? Ahsante sana.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhahiri kwamba Jimbo la Mtwara Vijijini linahitaji ujenzi wa shule za kidato cha tano na sita. Ni kweli kwamba tulishafanya tathmini na kuona kwamba katika kata zile 21 za Jimbo la Mtwara Vijijini kuna maeneo ambayo tumeshayatambua kwa ajili ya kuanza ujenzi wa madarasa ya kidato cha tano na sita, pia kujenga mabweni na maabara kwa zile shule ambazo zitakuwa na mchepuo wa masomo ya sayansi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mpango ambao tumeweka katika mwaka ujao wa fedha, sehemu mojawapo ambayo tumeipa kipaumbele ni kujenga madarasa ya kidato cha tano na sita katika Jimbo la Mtwara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa swali la pili, tunafahamu kuwa zipo shule nyingi ambazo zinahitaji kujenga uzio kwa ajili ya usalama, na ni jambo muhimu, lakini safari ni hatua, na kupanga ni kuchagua. Tumekubaliana kwamba, kwanza tuboreshe miundombinu ya elimu, wanafunzi waingie madarasani. Pili, tutakwenda sasa na mpango wa kujenga uzio katika shule zetu hizo. Kama haitoshi, halmashauri wenyewe pia wanaweza wakaanza kutenga fedha kwa awamu kupitia mapato ya ndani na kuanza kujenga uzio.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kumwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtwara Vijijini kuanza kutenga fedha kwenye bajeti zao kwa ajili ya kuanza ujenzi wa fence hiyo kwa awamu.

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. ARIF S. PREMJI aliuliza:- Je, Shule ngapi za kidato cha tano na sita zimejengwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 hadi kufikia robo ya pili?

Supplementary Question 2

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Tunapoelekea mwaka 2028, wanafunzi wote watamaliza, wale wa darasa la sita na darasa saba na tunaenda kwenye madarasa ya form four. Je, Serikali ina mpango gani wa kuona kwamba shule hizi za kidato cha tano na cha sita kuwa na shule za day ili kuongeza idadi ya wanafunzi kwenye maeneo yote ambayo wanafunzi wanaongezeka?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imefanya mpango mkakati kwamba tunatambua kuanzia Januari, 2028 tutakuwa na double cohort, kwa maana ya wanafunzi wa darasa la sita na la saba mwakani 2027, wote wataingia kidato cha kwanza Januari, 2028.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafahamu kwamba wanafunzi hawa watakwenda mpaka kidato cha nne na tutahitaji ongezeko la madarasa, shule na miundombinu mingine ya kidato cha tano na sita. Ninaomba kumhakikishia Mheshimiwa Boniphace Getere, Mbunge wa Bunda, kwamba Serikali katika mpango huo tumeweka eneo la kuhakikisha kwamba pia tutajenga shule, madarasa na miundombinu kwa kidato cha tano na sita ambazo zitaweza kuwachukua wanafunzi hawa wote ambao wataingia Januari, 2028.

Name

Esther Nicholas Matiko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Tarime Mjini

Primary Question

MHE. ARIF S. PREMJI aliuliza:- Je, Shule ngapi za kidato cha tano na sita zimejengwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 hadi kufikia robo ya pili?

Supplementary Question 3

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona. Halmashauri ya Mji wa Tarime tangu kuanza kwake ina shule moja tu ya kidato cha tano na cha sita, ambayo ni ya wavulana tu, ya Tarime Sekondari. Kwa kuwa nimekuwa muda mwingi nikizungumzia kuhusiana na shule ya Mogabiri Sekondari kupandishwa hadhi kuwa ya kidato cha tano na cha sita; na kwa kuwa miundombinu ya ujenzi wa mabweni na madarasa imeshakamilika. Je, Serikali haioni kwamba sasa hivi ni muda mwafaka wa kupandisha hadhi ya elimu katika Mji wa Tarime kwa kuanzisha Shule hii ya Sekondari ya Mogabiri kuwa na kidato cha tano na cha sita ili iweze kutoa elimu kwa wavulana na wasichana ndani ya Mji wa Tarime na wengine kutoka sehemu nje ya Tarime?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya vigezo vya kuanzisha shule za Kidato cha tano na sita ni idadi ya wanafunzi wa kidato cha nne ambao wanatarajia kuingia kidato cha tano; pili, ni umbali wa wanafunzi wanaohitaji kuingia kidato cha tano na sita kutoka shule nyingine; na tatu, ni upatikanaji wa eneo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaitumia nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge wa Tarime Mjini na wananchi wa Tarime kwa kujenga miundombinu katika shule hiyo ya kuanzia ili tuweze kupandisha hadhi kuwa kidato cha tano na sita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa suala hilo tumelichukua, tutalifanyia kazi haraka iwezekanavyo ili tuweze kupandisha hadhi shule hiyo baada ya kujiridhisha na vigezo, kufanya tathmini ya vigezo ili wanafunzi wa eneo hilo waweze kupata huduma kidato cha tano na sita.

Name

Anne Kilango Malecela

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Same Mashariki

Primary Question

MHE. ARIF S. PREMJI aliuliza:- Je, Shule ngapi za kidato cha tano na sita zimejengwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 hadi kufikia robo ya pili?

Supplementary Question 4

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru. Pamoja na kwamba Mheshimiwa Waziri amejibu kwa ujumla, lakini ninaomba kuuliza swali. Mimi nina Shule ya Sekondari ya Kimala ambayo ni high school ya wasichana tu. Hata hivyo, shule hii iko milimani, na ninakiri kwamba shule hii ni nzuri sana lakini haina uzio, na pale ilipo siyo mahali pazuri sana. Je, Serikali haioni kwamba ni vyema sasa wakaenda kuitembelea ile shule na kuona umuhimu wa kuweka uzio, ukizingatia kwamba ni shule ya wasichana watupu?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi, uzio katika shule zetu ni hitaji muhimu kwa ajili ya usalama wa watoto wetu wa kike, na pia wa kiume. Serikali inatambua umuhimu huo, na ndiyo maana katika kila mwaka wa fedha ziko shule ambazo tumeendelea kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya ujenzi wa fence, na pia tunaendelea na kujenga miundombinu mingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tumepokea hoja ya mama yangu, Mheshimiwa Anne Kilango Malecela. Tutashirikiana na Halmashauri ya Same kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri, na Serikali Kuu tutaona pale ambapo tutapata fursa ya kifedha kwa ajili ya kujenga fence hiyo, tutapeleka fedha kuhakikisha kwamba fence hiyo inajengwa na kuboresha usalama kwa watoto wetu wa shule hiyo.