Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Shaffin Ahmedali Sumar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uyui
Primary Question
MHE. SHAFFIN A. SUMAR aliuliza: - Je, lini Serikali itafanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Bwawa la Maji na Chujio katika Kata ya Shitage?
Supplementary Question 1
MHE. SHAFFIN A. SUMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru, na ninaishukuru sana Serikali kwa majibu mazuri. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa, huu upembuzi sasa unaelekea kutekelezwa na muda siyo mrefu, mradi utakuwa umekamilika. Je, nini mpango wa Serikali kusaidia zile kata ambazo zipo jirani na mradi huu, ambazo ni Kata ya Bukumbi na Igulungu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kwa kuwa, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ana nia njema sana ya kuwasambazia maji Watanzania mpaka kwenye vitongoji, na Kwa kuwa, sisi Mkoa wa Tabora tayari tuna Mradi wa Ziwa Victoria, na kwa kuwa, mradi huu umefika katika wilaya mbalimbali, ikiwemo Wilaya ya Tabora Manispaa ambapo kuna Bwawa la Igombe, je, nini mpango wa Serikali kuangalia vile vijiji vilivyopo jirani na Bwawa la Igombe ambapo kuna vijiji vya Kata yangu ya Ibiri na Usagala kuweza kupatiwa maji kwa sababu, bado mpango huo haujawafikia maeneo husika?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa ninampongeza kwa kusimamia vyema ajenda hii ya maji kwa ajili ya wananchi wake wa Uyui. Pia, ajenda hii inaenda sambamba kabisa na Sera ya Maji ya kuhakikisha kwamba, Watanzania wanapata huduma ya majisafi na salama. Bwawa hili la Shitage litaweza kuwafikia wananchi wa Bukumbi na Igulungu ambao Mheshimiwa Mbunge amesema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu, tutafanya usanifu wa kina. Baada ya hapo, tutafanya usanifu mwingine, kwa ajili ya miundombinu. Katika usanifu wa miundombinu hii sasa tutahakikisha Bukumbi pamoja na Igulungu wanakuwemo katika mradi huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye suala la pili kama ambavyo nimesema, linaendana na sera yetu ya maji. Pale ambapo bomba kuu linapita kushoto na kulia kilometa 12, sisi tunahakikisha vijiji husika vinapata huduma ya majisafi na salama. Tunatambua Serikali imeweka uwekezaji mkubwa wa kuleta maji ya Ziwa Victoria, ambayo yanapokelewa katika Bwawa la Igombe, yanaenda katika Wilaya ya Kaliua na Urambo. Tutahakikisha vijiji vilivyopo katika maeneo yaliyozunguka Bwawa la Igombe vinapata huduma ya majisafi na salama. Nakushukuru sana.
Name
Asha Salum Motto
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHAFFIN A. SUMAR aliuliza: - Je, lini Serikali itafanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Bwawa la Maji na Chujio katika Kata ya Shitage?
Supplementary Question 2
MHE. ASHA S. MOTTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Mradi wa Makonde, Mkoani Mtwara, ulipaswa kukamilika mwezi Machi, lakini hadi sasa mradi huu haujakamilika una 46% na mkandarasi hayupo site. Ni nini Kauli ya Serikali kuhusu ukamilishaji wa mradi huu Mkoani Mtwara? Ahsante.
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Asha, Mbunge kutoka Mkoa wa Mtwara. Kwanza kabisa, ninapenda kuipongeza sana Serikali ya Chama cha Mapinduzi, Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia kwa mapana yake Waheshimiwa Wabunge wanaposimama wanaongelea kuhusu malipo ya wakandarasi, maana yake ni madeni. Madeni ya wakandarasi yanaakisi uwekezaji mkubwa sana wa Serikali kuhakikisha kwamba tunatatua changamoto ya maji kwa wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii inaonesha ni dhamira thabiti ya Serikali kuweka fedha nyingi katika miradi ya maji ili kuhakikisha kwamba, changamoto inayokumba Watanzania katika kupata huduma ya majisafi na salama, inatatuliwa. Kwa hiyo, hii ni safari njema. Ninamtoa hofu katika miradi yote ambayo inaendelea, Mradi wa Makonde ni kati ya miradi ya miji 28 ambayo inaendelea kutekelezwa nchi nzima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamtoa hofu, tutaendelea kutatua changamoto awamu kwa awamu. Tutaendelea kupeleka fedha kuhakikisha kwamba, miradi hii inaendelea kukamilika ili iweze kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa Watanzania. Nakushukuru sana.
Name
Sara Msafiri Ally
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Mvomero
Primary Question
MHE. SHAFFIN A. SUMAR aliuliza: - Je, lini Serikali itafanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Bwawa la Maji na Chujio katika Kata ya Shitage?
Supplementary Question 3
MHE. SARA M. ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza na ninampongeza Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Kuna mradi mkubwa unaenda kutekelezwa Jimbo la Kilindi ambalo linapakana na Jimbo la Mvomero na chanzo cha maji cha mradi huu kinapatikana Kata ya Kibati iliyopo Jimbo la Mvomero, na hakuna majisafi na salama kwenye kata hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, nini mpango wa Serikali kuiingiza Kata hii ya Kibati, ili iweze kupata majisafi na salama kupitia mradi huu mkubwa wa shilingi bilioni 26 wa Kilindi?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru dada yangu Mheshimiwa Sara Msafiri, Mbunge wa Mvomero. Bahati nzuri Mvomero nimefanya ziara nyingi. Kata hii ambayo Mheshimiwa Mbunge ameigusia, ninaifahamu vizuri, na hicho chanzo ninakifahamu, kinatarajiwa kutoa huduma katika Jimbo la Kilindi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamtoa hofu Mheshimiwa Mbunge, kama ambavyo nimesema, Sera yetu ya Maji inazingatia mambo mawili. Wanaoishi katika chanzo ambacho kinatarajiwa kutoa huduma eneo fulani, wanatakiwa kuwa wanufaika namba moja kabla ya kuyapeleka maji katika maeneo mengine ambayo yametarajiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kata hiyo tutahakikisha kwamba, inaingizwa katika mpango wa kunufaika na maji ambayo yanatokana na kata yao. Nakushukuru sana.
Name
Eng. Johnston Johansen Mutasingwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukoba Mjini
Primary Question
MHE. SHAFFIN A. SUMAR aliuliza: - Je, lini Serikali itafanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Bwawa la Maji na Chujio katika Kata ya Shitage?
Supplementary Question 4
MHE. ENG. JOHNSTON J. MUTASINGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza swali la nyongeza. Kwanza ninapenda kutoa pole kwa wananchi wa Jimbo la Bukoba Mjini kwa maafa ya mvua inayoendelea sasa, mpaka tumepoteza watoto wetu wanane na wananchi wanaendelea kupoteza vitu vyao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kuuliza swali kwa Mheshimiwa Naibu Waziri. Je, ni lini Serikali itakamilisha upanuzi wa mtandao wa maji katika Jimbo la Bukoba Mjini ili wananchi wa Kitendaguro, Nyanga, Nshambya na Kishai waweze kupata maji kwa uhakika?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, Mhandisi. Ninampongeza sana kwa kazi nzuri anayoifanya pale Bukoba Mjini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamtoa hofu kwamba watu wetu wa BUWASA (Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba) wameanza kufanya tathmini, wamehakikisha kwamba wameweka mpango wa kuendelea kupanua ama kutanua distribution ya huduma ya maji awamu kwa awamu. Kwa hiyo, kulingana na fedha zitakavyokuwa zinapatikana, tuna uhakika hata wananchi katika maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyagusia huduma hiyo itafika bila kuwa na changamoto yoyote.