Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Paschal Inyasi Chinyele

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Primary Question

MHE. PASCHAL I. CHINYELE K.n.y. MHE. NAJMA MURTAZA GIGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuziboresha Barabara za Mitaa katika Jiji la Dodoma ikizingatiwa linakua kwa kasi?

Supplementary Question 1

MHE. PASCHAL I. CHINYELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Hata hivyo, nina maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa, Serikali imeamua kuhamia Dodoma, na kwa kuwa, Jiji la Dodoma linazidi kupanuka siku hadi siku, na kwa kuwa, katika baadhi ya kata za pembezoni, sasa ujenzi unafanyika kiholela kwa sababu hakuna barabara za mitaani, je, Serikali haioni kiwango hicho cha shilingi bilioni 10 kilichotengwa ni kidogo kulingana na hali halisi ya Jiji la Dodoma linavyopanuka na linahitaji barabara nyingi zaidi, kwamba walau Serikali ingeweka zaidi ya shilingi bilioni 10 ingekuwa na afadhali? Hilo ni swali la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Serikali imejipanga vipi kujenga barabara za lami katika mitaa ya Makole, Medeli, Matumbulu, Chigongwe, Mbabala, Mbalawala, Nala, pamoja na Mpunguzi?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze sana Mheshimiwa Paschal Chinyele, Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kwa kazi kubwa anayoifanya na kwa hakika anawasemea wananchi wa Dodoma Mjini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jiji la Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi na dhamira ya Serikali ni kuhakikisha tunajenga makao makuu ya nchi ya kisasa yenye barabara na miundombinu bora. Ndiyo maana katika kipindi cha miaka mitano Serikali imeendelea kujenga barabara za mitaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, tunafahamu, pamoja na fedha hizi ambazo zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara, Serikali imekuja na mpango mahsusi kwa ajili ya kujenga barabara katika Jiji la Dodoma. Mpango ambao unaitwa Dodoma Integrated Sustainable Transport Program ambao barabara za TANROADS pamoja na za TARURA zitajengwa kwa kiwango kikubwa. Hivi sasa Serikali iko hatua za manunuzi kwa ajili ya kumpata Consultant kwa ajili ya design ya mradi na kuhakikisha tunajenga barabara hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba lengo la Serikali ni kuendelea kuboresha barabara katika kata za pembezoni ambazo amezitaja: Kata ya Mbalawala, Mbabala, Matumbulu, Mpunguzi, Chigongwe na Nala. Hizi ni sehemu ya barabara ambazo zitakwenda kujengwa kuhakikisha kwamba jiji letu linakuwa na barabara bora, pamoja na barabara za mitaa yote. (Makofi)

Name

Jackson Gedion Kiswaga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalenga

Primary Question

MHE. PASCHAL I. CHINYELE K.n.y. MHE. NAJMA MURTAZA GIGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuziboresha Barabara za Mitaa katika Jiji la Dodoma ikizingatiwa linakua kwa kasi?

Supplementary Question 2

MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Barabara za Jimbo la Kalenga zimeharibika sana kutokana na mvua nyingi. Je, Serikali ina mpango gani wa haraka ili kupeleka sasa fedha ili tufanye ukarabati wa hizo barabara?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza Mheshimiwa Kiswaga, Mbunge wa Jimbo la Kalenga. Ni kweli wiki mbili zilizopita tulikuwa ziara katika jimbo lake, tumejionea barabara nyingi zimeharibika kutokana na mvua. Hali hii ipo katika majimbo yote kote nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kufanya tathmini ya mahitaji ya fedha kwa ajili ya marekebisho, ujenzi na ukarabati wa barabara hizi. Kama ambavyo Mheshimiwa Waziri wetu wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu alivyowasilisha juzi wakati wa bajeti yetu, zaidi ya shilingi bilioni 98 mpaka sasa zinahitajika, lakini tathmini bado zinaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, tunaendelea kufanya tathmini na Serikali inaandaa fedha kwa ajili ya ukarabati, na tayari shilingi bilioni 21.3 zimeshapelekwa katika majimbo mbalimbali hapa nchini kwa ajili ya kuendelea kufanya marekebisho, na zoezi hili ni endelevu.

Name

Agnesta Lambert Kaiza

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. PASCHAL I. CHINYELE K.n.y. MHE. NAJMA MURTAZA GIGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuziboresha Barabara za Mitaa katika Jiji la Dodoma ikizingatiwa linakua kwa kasi?

Supplementary Question 3

MHE. AGNESTA L. KAIZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kuniona. Barabara zote za mitaa yote ya Jimbo la Segerea ni mbovu, na nyingi hazipitiki kabisa. Nikitolea mfano wa barabara ya kutoka Kwa Bibi kuelekea Zahanati ya Segerea haipitiki kabisa, na hivi sasa imefungwa kabisa na wananchi wanakosa huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Swali langu kwa Serikali, je, Mheshimiwa Waziri yupo tayari kuambatana na mimi kwenye kipindi hiki cha Bunge la Bajeti, twende akajionee ndani ya Jimbo la Segerea ili aweze kuwapa neno wananchi wa Jimbo la Segerea. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na nimpongeze Mheshimiwa Agnesta. Barabara nyingi ni mbovu, siyo zote, zipo ambazo zinapitikia, lakini zilizo nyingi zina changamoto na Mheshimiwa Mbunge amesema mara kadhaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamhakikishia kabisa Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali hii inathamini wananchi wa Jimbo la Segerea. Kwa hiyo, tutaambatana naye, tutapanga muda mwafaka, tukakague barabara zile, lakini tuone namna nzuri ya kuhakikisha barabara zinajengwa ili wananchi wa Jimbo la Segerea waweze kufurahia matunda ya Serikali yao.

Name

Christina Solomon Mndeme

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. PASCHAL I. CHINYELE K.n.y. MHE. NAJMA MURTAZA GIGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuziboresha Barabara za Mitaa katika Jiji la Dodoma ikizingatiwa linakua kwa kasi?

Supplementary Question 4

MHE. CHRISTINA S. MNDEME: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya matengenezo na ujenzi wa barabara za mijini na vijijini, na kwa kuwa kipindi hiki cha mvua, barabara nyingi zimeharibika na hivyo kusababisha changamoto nyingi, je, Serikali ina mpango gani wa haraka wa ukarabati wa barabara za mijini na vijijini na hususan za Mkoa wa Tabora ambazo zimeharibika kwa mvua? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Ninampongeza sana Mheshimiwa Dkt. Christina. Ni kweli kwamba barabara nyingi zimekuwa zikijengwa, na katika bajeti yetu tumeona dhamira nzuri kabisa ya Serikali kuongeza bajeti mpaka shilingi trilioni 1.2 barabara za TARURA. Kwa hiyo, hii ni dhamira ya wazi ya Serikali kwamba inatambua umuhimu wa barabara na inaendelea kuongeza bajeti kwa ajili ya ujenzi barabara hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge, pamoja na ujenzi wa barabara hizi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kupitia TARURA, tunafanya tathmini ya kuboresha design ya barabara zetu, kama Mheshimiwa Waziri alivyosema katika kuhitimisha. Tunafikiria kuanza kuwa na concrete strips hasa kwenye maeneo ya milima, miteremko na yenye mvua nyingi ili tuweze kuwa na barabara zinazodumu ambazo hazitumii fedha kila mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mpango wa sasa ambao tunaendelea nao wa kuandaa fedha za dharura kwa ajili ya ukarabati wa barabara zilizoathirika na mvua, tutahakikisha barabara za Mkoa wa Tabora zinapewa kipaumbele ili wananchi wa Mkoa wa Tabora waweze kupata huduma bora za usafiri na usafirishaji. (Makofi)

Name

Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba kusini

Primary Question

MHE. PASCHAL I. CHINYELE K.n.y. MHE. NAJMA MURTAZA GIGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuziboresha Barabara za Mitaa katika Jiji la Dodoma ikizingatiwa linakua kwa kasi?

Supplementary Question 5

MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Muleba ni kati ya wilaya ambazo zina maeneo mengi oevu na barabara nyingi zimekatika. Kwa mfano, kutoka Runazi kwenda Kyebitembe mpaka daladala haziwezi kutoa huduma. Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha kwamba wilaya kama Muleba ambazo zina maeneo mengi oevu zinatengewa bajeti mbadala ili iweze kukarabati pindi mvua zinapoharibu barabara zetu? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Nimpongeze Dkt. Kikoyo Mbunge wa Muleba Kusini, na nimhakikishie tu kwamba Serikali inatambua, kutokana na tofauti za hali za kijiografia katika nchi yetu, yapo maeneo yenye mvua nyingi na ardhi oevu zaidi. Pia yapo maeneo yenye milima mingi zaidi. Kwa hiyo, Serikali inapitia utaratibu wa formula ya kugawa fedha za barabara kwenye majimbo na wilaya zetu ili fedha ziendane na hali ya kijiografia na kuhakikisha kwamba barabara zinajengwa kwa ufanisi mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Kikoyo, wakati formula hiyo itakapokuwa ipo tayari, tutahakikisha Jimbo la Muleba linapewa kipaumbele kinachostahili. (Makofi)

Name

Neema Peter Majule

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. PASCHAL I. CHINYELE K.n.y. MHE. NAJMA MURTAZA GIGA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuziboresha Barabara za Mitaa katika Jiji la Dodoma ikizingatiwa linakua kwa kasi?

Supplementary Question 6

MHE. DKT. NEEMA P. MAJULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, mvua za mwaka huu zimeharibu sana barabara nyingi za hapa Dodoma. Je, Serikali imejipanga vipi kujenga mitaro ya kudumu ili mwaka ambao unakuwa na mvua nyingi, uweze kunusuru barabara za Mkoa wa Dodoma, kwa maana hapa Wabunge wengi ndipo tunapoishi? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze sana Mheshimiwa Dkt. Neema Majule, msemaji mzuri sana wa wananchi wa Mkoa wa Dodoma na hakika wanawake wa Mkoa wa Dodoma wamepata mwakilishi wao katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jiji la Dodoma kwamba, Serikali katika mipango yake imeboresha design ya barabara zetu kwamba barabara yoyote inayojengwa lazima iwe na mifereji, tena mifereji ya kudumu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kujenga mifereji, tunafanya barabara ziishi kwa muda mrefu na kuepusha gharama za mara kwa mara za ukarabati. Kwa hiyo, tuna mpango huo katika barabara zote tunazoendelea kujenga, na zote ambazo tayari zimejengwa, nyingi zina mifereji na zile ambazo hazina mifereji tunaendelea kujenga mifereji ili barabara ziwe imara zaidi.