Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 11 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 116 | 2026-04-17 |
Name
Najma Murtaza Giga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. PASCHAL I. CHINYELE K.n.y. MHE. NAJMA MURTAZA GIGA aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kuziboresha Barabara za Mitaa katika Jiji la Dodoma ikizingatiwa linakua kwa kasi?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Najma Murtaza Giga, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jiji la Dodoma ni Makao Makuu ya nchi yetu, hivyo kumekuwa na ongezeko la watu na ukuaji wa kasi wa jiji, hivyo kuongeza mahitaji ya barabara za mitaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya barabara za mitaa ya Jiji la Dodoma, ambapo katika kipindi cha mwaka 2021/2022 hadi 2024/2025 jumla ya shilingi bilioni 59.6 zimetumika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, katika mwaka wa fedha 2025/2026 jumla ya shilingi bilioni 6.12 zimetumika kujenga na kukarabati barabara za lami za mitaa. Aidha, katika mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali imetenga shilingi bilioni 10.23 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara za mitaa za Jiji la Dodoma.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved