Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Asha Omar Rashid

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA OMAR RASHID aliuliza:- Je, lini Serikali itaongeza idadi ya Madaktari katika Hospitali za Wilaya ili kuboresha Huduma za Afya?

Supplementary Question 1

MHE. ASHA OMAR RASHID: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa maswali mazuri ya Serikali. Pia, nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suhulu Hassan, kipenzi chetu, kwa kutoa ajira 500 za madaktari Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, nataka kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha maslahi ya madaktari katika vituo vya kutolea huduma?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali namba mbili. Je, Serikali imejipangaje kuwapatia semina elekezi madaktari na watoa huduma, ili waweze kutumia lugha iliyo fasaha hasa wakati wakipokea wakina mama wakienda kujifungua hospitalini? (Makofi)

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Asha Omar kwa kuuliza maswali ambayo yanagusa jamii yetu, wakina mama wetu, na watumishi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kujali maslahi ya watumishi wetu kote nchini. Katika mwaka wa fedha 2025/2026 na 2026/2027 tumetenga jumla ya shilingi bilioni 13 kwa ajili ya kulipa on calls, yaani madaktari wanapoitwa kazini, kwenda kufanya kazi zao za dharura. Pia, zimetengwa shilingi bilioni 10 za kulipa stahiki zao za likizo. Vilevile, tumetenga zaidi ya shilingi bilioni 7.5 kwa ajili ya kulipa stahiki zao za uhamisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Ninaomba tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI pamoja na Wizara ya Afya, tumeendelea kushirikiana kutoa miongozo na tumekuwa tukisisitiza sana madaktari wetu watoa huduma kuendelea kutoa lugha za staha, lugha za mawasiliano bora kazini, ili kuweza kuwahudumia wananchi wetu, kuwahudumia mama zetu, hasa wale wajawazito.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akituelekeza sana katika hili, kuendelea kuwa wazalendo na kuwatibu kwa lugha stahiki wagonjwa wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha. (Makofi)

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Hanang'

Primary Question

MHE. ASHA OMAR RASHID aliuliza:- Je, lini Serikali itaongeza idadi ya Madaktari katika Hospitali za Wilaya ili kuboresha Huduma za Afya?

Supplementary Question 2

MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, ni lini Serikali itapeleka wataalamu na vifaa tiba kwa zahanati na vituo vya afya vilivyokamilika katika Jimbo la Hanang?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kupeleka vifaa tiba na madaktari katika hospitali zote nchini. Kwa hiyo, nimwelekeze Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hanang, kuendelea kupeleka watumishi katika zahanati yetu hii na kuendelea kutoa huduma kwa mama zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.

Name

Adonis Alfred Bitegeko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba Kaskazini

Primary Question

MHE. ASHA OMAR RASHID aliuliza:- Je, lini Serikali itaongeza idadi ya Madaktari katika Hospitali za Wilaya ili kuboresha Huduma za Afya?

Supplementary Question 3

MHE. ADONIS A. BITEGEKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kunipa nafasi. Tunashukuru kwamba Serikali imejenga kituo cha afya katika Kata ya Bumbire iliyopo Kisiwani, lakini hiki kituo cha afya kinakabiliwa na upungufu mkubwa wa wataalamu wakiwemo madaktari, wafamasia, wataalamu wa maabara na wataalamu wa dawa za usingizi. Je, ni lini Serikali itapeleka wataalamu ili kuwezesha kutoa huduma bora katika kituo hicho?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwahidi mbele ya Bunge lako Tukufu, mimi na yeye baada ya hapa tutakaa, kwa kuwa amesema kuna upungufu mkubwa, basi tuchukue hatua stahiki za dharura angalau tuanze na reallocation ya watumishi walioko ndani ya halmashauri waende wakatoe huduma kwa wananchi wetu kule visiwani.

Name

Yagi Maulid Kiaratu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Singida Mjini

Primary Question

MHE. ASHA OMAR RASHID aliuliza:- Je, lini Serikali itaongeza idadi ya Madaktari katika Hospitali za Wilaya ili kuboresha Huduma za Afya?

Supplementary Question 4

MHE. YAGI M. KIARATU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa nafasi. Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Singida ina daktari bingwa mmoja tu wa wanawake. Haina daktari bingwa wa watoto, haina daktari bingwa wa magonjwa ya ndani, inakosa wataalamu wa usingizi, na pia wataalamu wa mionzi hakuna kabisa. Bahati nzuri Mheshimiwa Naibu Waziri alikuja akaona hali ya hospitali ya Manispaa ya Singida ilivyo mbaya kwa sababu haina madaktari.

MWENYEKITI: Swali.

MHE. YAGI M. KIARATU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini Serikali itaona umuhimu wa kupeleka wataalamu hao ili kutoa huduma bora kwa wananchi wa Manispaa ya Singida?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi na Mheshimiwa Mbunge tulifanya ziara katika hii hospitali yetu. Ni kweli baadhi ya wataalamu tuliona upungufu huo na Serikali tulipokea. Hata hivyo, pale pale nilimwelekeza Mkurugenzi awasiliane na DMO kwanza kuangalia kutoa ajira za mkataba kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma za mionzi katika hospitali yetu hii ya Singida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo la Singida kwamba, tutaendelea kuelekeza wataalamu hasa wale kwenye zile taaluma ambazo ni chache, tuna uhaba kuendelea kupeleka wataalamu katika hii hospitali yetu ambayo ni nzuri, inahudumia wananchi wengi na ina majengo bora.

Name

Dr. Regina Christopher Malima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA OMAR RASHID aliuliza:- Je, lini Serikali itaongeza idadi ya Madaktari katika Hospitali za Wilaya ili kuboresha Huduma za Afya?

Supplementary Question 5

MHE. DKT. REGINA C. MALIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, Serikali ina mpango gani wa kuweka utaratibu wa kuwapatia nafasi wanafunzi wanaosoma udaktari nje ya nchi pindi wanaporejea ili warejee na wasaidie kupunguza changamoto ya madaktari iliyopo katika hospitali zetu za wilaya?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua madaktari wanaopata mafunzo nje ya nchi na wanaporudi huwa kwanza wanapokelewa na TCU kuweza ku-verify vyeti vyao. Pia wanapokelewa na Wizara yetu ya afya, wanapitia katika mafunzo ya internship katika hospitali zetu mbalimbali nchini, baada ya hapo huwa wanaomba ajira kama wanavyoomba wengine na wameendelea kuajiriwa katika hospitali zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tutaendelea kuajiri madaktari wanaosoma nje na ndani ya nchi kwa maana ya kwamba wote wanapata mafunzo sawa, na wanaporejea nchini huwa bado wanapewa mafunzo pia na uzalendo wa kutoa lugha stahiki kwa wananchi wetu.

Name

Husna Juma Sekiboko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA OMAR RASHID aliuliza:- Je, lini Serikali itaongeza idadi ya Madaktari katika Hospitali za Wilaya ili kuboresha Huduma za Afya?

Supplementary Question 6

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. Kwa kuwa tunafahamu kwamba Serikali inaajiri madaktari kulingana na upatikanaji wa fedha, naomba idadi ya madaktari wanaajiriwa katika mpango wa Serikali kwa kila mwaka wa bajeti?

Name

Husna Juma Sekiboko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, sina takwimu sahihi, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Sekiboko kwamba, uhitaji tunaopata kutoka katika vituo vyetu vya afya ndiyo tunaufanyia kazi. Hili aliliona Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanza kuajiri wataalamu wa afya 5,000 ili kuhakikisha tunatoa huduma katika vituo vyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaendelea kuajiri madaktari, na kuna kipindi tunaelekeza madaktari wa mkataba waajiriwe ili kwenda kuhakikisha tunaendelea kutoa huduma.

Name

Japhael Masanja Lufungija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ulyankulu

Primary Question

MHE. ASHA OMAR RASHID aliuliza:- Je, lini Serikali itaongeza idadi ya Madaktari katika Hospitali za Wilaya ili kuboresha Huduma za Afya?

Supplementary Question 7

MHE. JAPHAEL M. LUFUNGIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa nafasi. Ninapenda kuuliza, Jimbo la Uliyankulu ni jimbo ambalo liko mbali sana na huduma za hospitali ya wilaya, lakini lina vituo vya afya vitano. Kituo cha Afya cha Kashishi hakina MD hata mmoja, na Kituo cha afya cha Mwongozo, hakina MD hata mmoja. Hata hivyo vituo vya afya vya Ilege, Uyoa pamoja na Ulyankulu vina MD mmoja mmoja. Nini mpango wa Serikali wa kuhakikisha kwamba MDs wanapatikana kwenye hayo maeneo?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kumjibu Mheshimiwa Mbunge wa Ulyankulu kaka yangu, na mara zote tumekuwa tukizungumza haya, na alishakuja pale Wizarani, TAMISEMI tukakaa vizuri kuangalia namna gani tuwapate hawa MDs wawili angalau waende wakaendelee kutoa huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo la Ulyankulu, sisi kama Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, tutaendelea kuelekeza wataalamu wetu ili waendelee kutoa huduma katika vituo vyetu vya afya.

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. ASHA OMAR RASHID aliuliza:- Je, lini Serikali itaongeza idadi ya Madaktari katika Hospitali za Wilaya ili kuboresha Huduma za Afya?

Supplementary Question 8

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Kituo cha Afya Unyali, Kituo cha Afya Mgeta, Kituo cha Afya Behinga ambacho ni kipya, watumishi hawapo, kuna watumishi wawili, watatu. Ni lini sasa mtapeleka watumishi kwenye hayo maeneo?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, nimepokea changamoto za upungufu wa watumishi hao kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI. Mimi na Mheshimiwa Mbunge tutakaa chini kuangalia namna gani ya kuwapata hawa MD ili tuweze kuwaelekeza katika vituo vya afya ambavyo Mheshimiwa Getere ameviorodhesha.