Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 11 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 114 | 2026-04-17 |
Name
Asha Omar Rashid
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ASHA OMAR RASHID aliuliza:-
Je, lini Serikali itaongeza idadi ya Madaktari katika Hospitali za Wilaya ili kuboresha Huduma za Afya?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Asha Omar Rashid, Mbunge wa Viti Maalum, akitokea Kaskazini Pemba lakini pia huyu ni Mjumbe wa Kamati ya TAMISEMI.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kutenga bajeti na kuajiri watumishi wa kada mbalimbali za afya nchini. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2025/2026 jumla ya watumishi wa kada mbalimbali za afya 37,921 wameajiriwa. Wataalamu hao ni pamoja na madaktari (MD - Medical Doctors) 1,985 pamoja na kada nyingine 35,936. Aidha, zaidi ya 55% ya watumishi hawa wamepangwa katika hospitali za Halmashauri kote nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imeajiri watumishi 5,000 wa kada mbalimbali za afya ambapo watumishi 134 ni madaktari ambao wamepangiwa kutoa huduma kwenye Hospitali na vituo vya afya vinavyotoa huduma za upasuaji wa dharura.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga bajeti na kuajiri Madaktari na kuwapanga katika hospitali zenye upungufu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved