Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Happiness Daniel Ngwando
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAPPINESS D. NGWANDO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kutengeneza barabara za usalama mipakani ili kuwezesha vyombo vya ulinzi na usalama kufanya doria?
Supplementary Question 1
MHE. HAPPINESS D. NGWANDO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa barabara hizi zimekuwa na umuhimu sana hasa kwa wananchi wanaoishi mipakani kiuchumi pamoja na ulinzi wao; kwa mfano, tukiongelea Dapoli - Mbinga, Mitomoni Songea, Magazini - Namtumbo kuelekea Wenje na Nalasi – Tunduru, je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka fedha kwa haraka ili kuzuia watu wabaya na wahalifu ambao hawaitakii mema nchi yetu? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Barabara ya Mtwara - Pachani kuelekea Nalasi Lingusenguse imefanyiwa upembuzi yakinifu kuanzia mwaka 2022 na usanifu wa kina. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kwenye barabara hiyo ukizingatia ni barabara ambayo wananchi wake wanalima ‘pesa’ nikimaanisha inalima korosho pamoja na ufuta, lakini kilometa 200 kutoka kwenye hospitali ya Kata moja mpaka kufika kwenye Wilaya ndiyo mama mjamzito anaweza kufika huko?
Mheshimiwa Spika, je, Serikali haioni umuhimu wa barabara hii kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma hususan Wilaya ya Namtumbo na Tunduru? Ahsante. (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema katika jibu la msingi, kipaumbele cha kwanza kwa barabara za mipakani ni kuhakikisha kwamba nchi yetu inakuwa salama, kwa maana ya kusaidia vyombo vya usalama kuweza kupita muda wote inapohitajika na ndiyo maana tunaziimarisha, pale ambapo hatujazifungua, tunahakikisha kwamba tunazifungua.
Mheshimiwa Spika, ninatambua pia zikishajengwa inakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi ambao wanazitumia hizo barabara kwa shughuli zao za kawaida ikiwa ni pamoja na kiuchumi na za kijamii. Kwa hiyo, nimhakikishie Mbunge kwamba, Serikali kama tulivyosema, tutaendelea kuziimarisha na kuzifungua na kuhakikisha kwamba zinapitika muda wote.
Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la pili, ni kweli kwamba tuna barabara hiyo ya Mtwara - Pachani - Nalasi kwenda Tunduru yenye urefu wa kilometa 300, barabara ambayo tumeshakamilisha usanifu, lakini imekuwa ikiombewa fedha, na kwa kuwa bajeti bado haijaruhusu kuijenga barabara yote, tunachofanya kwanza ni kuhakikisha inapitika muda wote na maeneo yote yale korofi, tunachokifanya sasa hivi ni kuhakikisha kwamba tunajitahidi kujenga ama zege, ama lami, ama kama kuna daraja ambalo limekwama, huo ndiyo mkakati ambao tunasema tuijenge ili iweze kupitika kwa muda wote, tukiwa tunatafuta fedha kuijenga barabara yote kwa kiwango cha lami. Ahsante.
Name
Suma Ikenda Fyandomo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAPPINESS D. NGWANDO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kutengeneza barabara za usalama mipakani ili kuwezesha vyombo vya ulinzi na usalama kufanya doria?
Supplementary Question 2
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwanza niwape pole sana wananchi wa Wilaya ya Rungwe kwa maporomoko makubwa yaliyotokea, yaliyosababishwa na mvua iliyopelekea ndugu zetu 21 kutangulia mbele ya haki, ‘ndaga wana Rungwe, ndaga mgonie upepo.’
Mheshimiwa Spika, mvua ile ilisababisha kuporomoka kwa daraja kubwa sana liitwalo Lubangalala. Daraja hilo linaunganisha Kata kwa upande wa Rungwe Kata ya Ikuti, Lupepo, Iponjola, Kyimo na Kiwira. Daraja hilo pia linaunganisha na Wilaya ya Ileje ambalo Kata za upande wa Ileje ni Kata za Ngulugulu, Ngulilo, Sange, Lubanda na Luswisi.
Mheshimiwa Spika, naishukuru sana Serikali baada ya kuona daraja hilo ni la muhimu, Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ilituma fedha kwa haraka ili kuhakikisha daraja hilo linajengwa. Je, ni lini daraja hilo litakamilika kwa umuhimu huo? Ahsante. (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kwanza nami niungane na Mbunge kuwapa pole sana wananchi wa Mkoa wa Mbeya na hasa Wilaya ya Rungwe ambao walipata changamoto ya maporomoko kutokana na kunyesha kwa mvua kubwa katika eneo hilo.
Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba barabara hiyo ambayo inatoka Ileje kwenda Rungwe kuna daraja lilikatika ambalo lilikata mawasiliano kati ya Wilaya hizo mbili. Kilichofanyika kwanza, ilikuwa ni kujenga kivuko cha dharura walau watu wapite kwa miguu na baada ya hapo Serikali baada ya kuona changamoto hiyo iliwapa maelekezo Meneja wa Mkoa wa Mbeya kuhakikisha kwamba anarejesha mawasiliano haraka.
Mheshimiwa Spika, tunavyoongea hivi, daraja la muda ambalo litapitisha magari mpaka jana limekamilika. Kwa hiyo, tuna hakika baada ya muda mfupi, baada ya taratibu zote za kihandisi itakapokuwa imekaa, wataanza kupita kwenye hilo daraja.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tumechukua hatua kwa haraka kuhakikisha kwamba tunaunganisha mkoa wa Mbeya na Songwe lakini pia Wilaya ya Ileje na Wilaya ya Rungwe ambayo ni muhimu sana hiyo barabara kwa maisha yao. Ahsante. (Makofi)
Name
Abdallah Jafari Chaurembo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chamazi
Primary Question
MHE. HAPPINESS D. NGWANDO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kutengeneza barabara za usalama mipakani ili kuwezesha vyombo vya ulinzi na usalama kufanya doria?
Supplementary Question 3
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Barabara ya kutoka Rangitatu, Majimatitu mpaka Mbande ni barabara ambayo imezidiwa sana na msongamano wa magari, kiasi kwamba mpaka bodaboda sasa zinapanga foleni. Je, Serikali ina mpango gani wa kuipanua barabara hiyo ili wananchi waweze kupita kwa urahisi? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Jiji la Dar es Salaam, sehemu kubwa ina misongamano mikubwa. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tumeshafanya study ya kuhakikisha kwamba sehemu zote ambazo zina changamoto zinajengwa upya, kwa maana ya kuongeza upana wa barabara ama kufanya njia nne.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Dar es Salaam, hasa wa maeneo ambayo ameyataja Mheshimiwa Chaurembo, nayo ni maeneo ambayo tayari yameshafanyiwa design, kwa maana ya kuijenga kwa njia nne ama kuipanua ili iweze kupunguza foleni ambayo ipo katika hayo maeneo.
Name
Christina Solomon Mndeme
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAPPINESS D. NGWANDO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kutengeneza barabara za usalama mipakani ili kuwezesha vyombo vya ulinzi na usalama kufanya doria?
Supplementary Question 4
MHE. CHRISTINA S. MNDEME: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali imekuwa ikiendelea kuboresha miundombinu ya barabara nchi, je, Serikali ina mango gani wa kujenga barabara kwa kiwango cha Puge kwenda Ziba mpaka Choma ili kuwaondolea changamoto ya ubovu wa barabara wananchi na hususan wanawake wanapokwenda kupata huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa ya Nkinga iliyopo Wilayani Igunga?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, hii barabara ilikuwa kwanza haijafanyiwa usanifu, tulikuwa tunakamilisha usanifu. Pamoja na hayo, tulishapata kibali cha kuanza kujenga walau kwa awamu, na tutaanza pande zote mbili. Tulikubaliana hivyo, tuanze pande mbili, huku na huku. Hivi ninavyosema, sasa hivi tunaanza na kilometa 12 kujenga kwa kiwango cha lami. Kwa hiyo, kibali kilishatolewa.
Name
Bonnah Ladislaus Kamoli
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Segerea
Primary Question
MHE. HAPPINESS D. NGWANDO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kutengeneza barabara za usalama mipakani ili kuwezesha vyombo vya ulinzi na usalama kufanya doria?
Supplementary Question 5
MHE. BONNAH L. KAMOLI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Ninataka nimwulize Mheshimiwa Naibu Waziri, je, wana mpango gani na barabara ya Kinyerezi ambayo inapita Bonyokwa ambayo wameanza kutengeneza, lakini sasa haiko kwenye matengenezo na mkandarasi hayupo?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ninachofahamu ni kwamba, huyu mkandarasi ameshalipwa fedha, na mkandarasi ambaye yuko site ndiye anayetakiwa afanye hayo matengenezo, kwa sababu ni suala la kiutendaji.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nichukue nafasi hii kumwelekeza Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam ahakikishe anasimamia; na kwa kuwa mvua zinanyesha, ahakikishe anamsimamia mkandarasi na kufanya marekebisho, ikiwa ni pamoja na kukarabati diversion ili wananchi wa eneo hilo waweze kupita kwa amani na usalama.
Name
Edibily Kinyoma Kazala
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kasulu Vijijini
Primary Question
MHE. HAPPINESS D. NGWANDO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kutengeneza barabara za usalama mipakani ili kuwezesha vyombo vya ulinzi na usalama kufanya doria?
Supplementary Question 6
MHE. EDIBILY K. KINYOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali la nyongeza. Je, ni lini Serikali itaanza kujenga Barabara ya Uvinza – Kasulu kwa kiwango cha lami, ikizingatiwa ni ahadi ya Mheshimiwa Rais?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Ni kweli Barabara ya Uvinza kwenda Kasulu ina kama kilometa 60 hadi 62. Tumeshakamilisha usanifu. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ahadi ya Mheshimiwa Rais ni kipaumbele. Sisi kama Wizara ya Ujenzi na TANROADS tumeichukulia hii barabara kwa kipaumbele kikubwa sana, kwa sababu ndiyo barabara ambayo inatoka Tunduma – Sumbawanga – Mpanda – Uvinza – Kasulu – Kibondo hadi Nyakanazi.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninavyoongea sasa hivi, hicho kipande ndicho pekee ambacho kitakuwa kimebaki hakijajengwa kwa kiwango cha lami. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa Serikali inatafuta fedha ili kuhakikisha kwamba hicho kipande tumekikamilisha ili tuweze kukamilisha hiyo barabara yote ambayo ni T9.