Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Maryam Azan Mwinyi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Chake Chake
Primary Question
MHE. MARYAM AZAN MWINYI aliuliza: - Je, Serikali inachukua hatua gani kuwawezesha Wananchi hususan Vijana na Wavuvi wadogo kushiriki kikamilifu katika uchumi wa buluu?
Supplementary Question 1
MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza: Je, Serikali inashirikiana vipi na sekta binafsi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ili kuongeza fursa kwa wanawake katika uchumi wa bluu?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, ni vigezo gani vinatumika kupima mafanikio ya wananchi wanaoshiriki katika uchumi wa bluu? (Makofi)
Name
Ng'wasi Damas Kamani
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana. Ninampongeza sana Mheshimiwa Maryam Azan Mwinyi, kwanza kwa kuaminiwa na wanawake waliompa ridhaa ya kuwepo Bungeni hapa, lakini kwa kuendelea kupambana kwa maslahi mapana ya wanawake hawa.
Mheshimiwa Spika, katika swali lake la kwanza kuhusu nia na madhumuni ya sekta ya Serikali yetu ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali ya Awamu ya Sita na maelekezo mahsusi ya Rais ni kwamba, tuendelee kuziwezesha na kuzilea sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali na kushirikiana nayo kwa karibu sana katika sekta zetu.
Mheshimiwa Spika, nasi katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi hatupo nyuma, katika sekta yetu ya uvuvi, tunaendelea kuhakikisha kwamba tunazisogeza sekta binafsi na taasisi zetu za kifedha hasa mabenki, kuendelea kuwapunguzia vikwazo mbalimbali katika utendaji wao wa kazi ili kuhakikisha kwamba tunawanyanyua na kuwapa fursa nyingi zaidi hasa wanawake ili kuhakikisha kwamba wananyanyua uchumi wao na kushiriki katika sekta yetu ya uvuvi.
Mheshimiwa Spika, pia katika swali lake la pili la kuhusu vigezo gani tunatumia ili kupima maendeleo au upandaji wa sekta yetu ya uvuvi katika makundi haya maalum; tumeendelea kufanya kazi na vijana, wanawake na makundi maalum kwa karibu sana na kuchukua takwimu kwa kila mwaka, kuangalia namna gani tumewawezesha, kuwafuatilia kwa karibu kuhakikisha kwamba uwezeshaji tunaowapa unazaa matunda.
Mheshimiwa Spika, hivyo, tunazo takwimu za kutosha Wizarani kuona kwamba kila mwaka kadri tunavyotoa uwezeshaji huu na kadri Serikali inavyotenga bajeti, basi fedha hizi zinavyowafikia wanufaika hawa zinawapa manufaa yanayostahili.
Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved