Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 6 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 54 | 2026-04-10 |
Name
Maryam Azan Mwinyi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Chake Chake
Primary Question
MHE. MARYAM AZAN MWINYI aliuliza: -
Je, Serikali inachukua hatua gani kuwawezesha Wananchi hususan Vijana na Wavuvi wadogo kushiriki kikamilifu katika uchumi wa buluu?
Name
Ng'wasi Damas Kamani
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana. Kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ninaomba nijibu swali la Mheshimiwa Maryam Azan Mwinyi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza mikakati mbalimbali ya kuwawezesha wananchi, hususan vijana na wavuvi wadogo, kushiriki kikamilifu katika uchumi wa bluu kwa lengo la kuongeza ajira, kipato, na mchango wa sekta ya uvuvi katika uchumi wa Taifa. Serikali inaendelea kutekeleza Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora, ambapo katika mwaka wa fedha 2025/2026 Wizara imepokea kiasi cha shilingi bilioni 30.7 (shilingi bilioni 25.9 katika Uvuvi na shilingi bilioni 4.75 katika Mifugo), kwa ajili ya kuwawezesha wavuvi wadogo pamoja na vijana katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mheshimiwa Spika, aidha, kupitia Programu hii ya BBT, vijana 308 kutoka mikoa yote nchi nzima wamepatiwa mikopo isiyo na riba na yenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeza miradi ya ufugaji wa samaki kwenye vizimba, ufugaji wa majongoo bahari, unenepeshaji kaa na kilimo cha mwani.
Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) inaendelea kutekeleza zoezi la utoaji wa mikopo isiyo na riba na yenye masharti nafuu kwa wavuvi wadogo, wakiwemo vijana, kwa kuwawezesha kupata nyenzo za uvuvi ikiwemo maboti ya kisasa pamoja na nyavu za uvuvi.
Mheshimiwa Spika, ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved