Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Charles Mhando Njama
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Korogwe Mjini
Primary Question
MHE. CHARLES M. NJAMA K.n.y. MHE. MABULA J. MAGANGILA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza kutumia rasilimali zake kama dhamana, ili Wafanyabiashara wa Kitanzania waweze kukopesheka zaidi?
Supplementary Question 1
MHE. CHARLES M. NJAMA: Mheshimiwa Spika, ahsante, ninapenda kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa, wananchi wengi wa Jimbo la Msalala wamejiajiri na kuajiri watu wengi katika uchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu na wamekuwa wakishindwa kukua kufikia uchimbaji wa kati na mkubwa kwa kukosa mitaji mikubwa na nafuu, je, ni lini Mheshimiwa Waziri utakuwa tayari kukutana na wafanyabiashara wa Msalala, ili kuwapatia elimu ya namna wanavyoweza kunufaika na mfuko huu wa dhamana? (Makofi)
Name
Laurent Deogratius Luswetula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. LAURENT D. LUSWETULA): Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza nachukua fursa hii kumpongeza sana Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mheshimiwa Mabula Johnson Magangila, kwanza kwa kuendelea kupigania haki za wafanyabiashara na wachimbaji wadogo wadogo wa madini ya dhahabu ndani ya Jimbo lake la Msalala.
Mheshimiwa Spika, katika swali hilo la nyongeza, ninapenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Msalala kwamba, Wizara ya Fedha, kupitia Ofisi ya Waziri, tuko tayari. Kabla ya kwisha kwa Bunge hili la Bajeti, tutakuwa tumefika katika Jimbo la Msalala kuongea na wafanyabiashara na wachimbaji wadogo wadogo wa madini ya dhahabu kuwapa elimu hii ya Mifuko ya Dhamana, ambayo ni hitaji kubwa kwa wafanyabiashara hao, ili waweze kupata mikopo hiyo kwa masharti nafuu na riba ndogo zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ahsante. Ninaomba... (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved